NIJUZE NIJUZE Author
Title: NYAKATI NGUMU HUPITA - ALI KAMWE
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Licha ya kipigo kutoka kwa MC Alger, Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe, ameonyesha matumaini makubwa na kuhimiza m...

Licha ya kipigo kutoka kwa MC Alger, Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe, ameonyesha matumaini makubwa na kuhimiza mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuendelea kuiunga mkono. Kamwe amesema kuwa licha ya matatizo yaliyopo, bado kuna nafasi ya kufufuka na kuonyesha ufanisi katika mechi zilizobaki.

Yanga ilipokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa MC Alger, ikiwa ni kipigo cha pili mfululizo kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara, hali ambayo imewaweka chini kabisa kwenye msimamo wa Kundi A.

Kamwe amekiri wazi kwamba Yanga inapata changamoto kubwa kwa sasa, lakini amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa wakati mgumu huu utapita, na kwamba wanapaswa kuendelea kuwa na imani na timu yao.

"Matokeo haya siyo ya kufurahisha na hatukutarajia kupoteza, lakini ndiyo hali ya mchezo. Huwezi kuingia kwenye michuano mikubwa kama hii ukidhani kila wakati utashinda. Lengo letu lilikuwa kushinda, lakini mpira una wakati wa furaha na wakati wa huzuni. Sasa tuko kwenye kipindi kigumu, lakini hii ni sehemu ya mchezo wa soka," alisema Kamwe.

Aliendelea kusema kwamba hata timu kubwa duniani kama Manchester City inapitia wakati mgumu, hivyo siyo jambo la kushangaza.

“Kikubwa ni kuweza kurudi imara. Hii hali isiyo ya kuridhisha haipaswi kuwa endelevu. Tunaamini kwa nguvu ya taasisi yetu na mafanikio ya zamani, tutarudi tena kwenye kiwango chetu cha juu,” alisema Kamwe, akisisitiza kwamba licha ya uchungu wa matokeo hayo, ni muhimu kukubaliana na hali halisi kwani matokeo mabaya yanaweza kutokea kwa timu yoyote.

Kamwe pia alisisitiza umuhimu wa mashabiki na wanachama kuwa watulivu katika kipindi hiki cha changamoto, akiongeza kuwa "nyakati hizi zinapima nguvu na uvumilivu wa kila mmoja. Tunahitaji umoja na msaada wa kila mmoja ili tuweze kurudi kwenye kiwango cha ushindani. Tunahitaji pointi 12 kutoka mechi zilizobaki ili tuweze kusonga mbele na tutazipata ikiwa tutaendelea kupigana."


Kikosi cha Yanga kimefika nyumbani leo, kikiwa na takribani siku tatu za maandalizi kabla ya kuelekea Lubumbashi kwa mchezo mkubwa dhidi ya TP Mazembe, utakaopigwa Disemba 14.

Kamwe anasema kuwa Yanga inahitaji kushinda au kupata matokeo ya sare katika mchezo huo ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kuendelea, kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa Dar es Salaam wiki mbili baadaye.

About Author

Advertisement

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top