NIJUZE NIJUZE Author
Title: MASHABIKI WAFURIKA RUANGWA KUISAPOTI YANGA SC
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mamia ya mashabiki wa Yanga wamesafiri hadi Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, ili kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu kati ya timu yao ya Yanga na ...

Mamia ya mashabiki wa Yanga wamesafiri hadi Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, ili kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu kati ya timu yao ya Yanga na Namungo FC, utakaochezwa leo katika Uwanja wa Majaliwa.

Mchezo huu unachukuliwa kuwa wa muhimu kwa Yanga, kwani unakuja baada ya timu hiyo kupoteza mechi tatu mfululizo, na sasa hakuna nafasi tena ya kupoteza alama.

Hadi sasa, Yanga na Namungo zimekutana mara kumi kwenye Ligi Kuu, ambapo Yanga imefanikiwa kushinda mechi tano na kupata sare tano, huku Namungo ikikosa ushindi katika mechi yoyote.

Katika mechi tano za ushindi, Yanga imeibuka na ushindi mara mbili ugenini na mara tatu nyumbani, huku ikipata sare mbili nyumbani na tatu ugenini.

Mchezo huu wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku Yanga ikijitahidi kurekebisha makosa ya nyuma.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top