CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MANISPAA YA LINDI

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Juma Mnwele, ametangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mnwele alibainisha kuwa kati ya nafasi 1,954 za uongozi zilizoshindaniwa na vyama 7 vya siasa, matokeo yanaonyesha ushindi mkubwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho kimeshinda viti 1,931, sawa na asilimia 98.82 ya jumla ya nafasi zote.

Vyama vingine vilivyoshiriki katika uchaguzi huo ni pamoja na ACT Wazalendo, ambacho kimeshinda nafasi 21, sawa na asilimia 1.07; CHADEMA, ambacho kilipata ushindi wa nafasi 2, sawa na asilimia 0.10; na CUF kilichoshinda nafasi 1, sawa na asilimia 0.05. Vyama vya CHAUMA na NCCR Mageuzi havikupata viti vyovyote katika uchaguzi huu.

 


Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post