RC LINDI AFUNGUA JENGO LA OFISI YA UHAMIAJI LINDI

 

Jengo jipya la Ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Lindi limefunguliwa leo hii April 26, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainab Telack

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainab Telack amezindua jengo la Ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Lindi leo hii katika sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 59 Muungano wa Tanzania.

Bi Zainab ameipongeza Wizara ya mambo ya ndani kwa kuweza kujenga jengo hilo ambalo litarahisisha huduma katika mkoa huu kwa wananchi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Bi Zainab amesema

“Imekuwa bahati kubwa leo hii kuzindua jengo hili kwani Linaenda kupendezesha mji wetu lakini pili linakwenda kufanya urahisi wa utendaji kazi wa jeshi letu la Uhamiaji”

 Jengo Hilo limegharimu kiasi cha Tsh 2,228,396,218.46

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post