NIJUZE NIJUZE Author
Title: RIVERS UNITED WAANZA SAFARI YA DAR ES SALAAM
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Achana na taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii zilizodai kuwa Rivers United wanakabiliwa na ukata na hivyo wanaweza kuwasili nchin...

Achana na taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii zilizodai kuwa Rivers United wanakabiliwa na ukata na hivyo wanaweza kuwasili nchini Jumamosi na kuondoka siku ya Jumatatu baada ya mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili

Wachezaji wa River United wakiwa Airpot Nigeria tayari kwa kuanza safari ya Kuja Dar es Salaam kuwakabili Young Africans

Hizo ni mbinu tu wanajaribu kutumia ili ionekane kama wamekata tamaa na mchezo wa marudiano

Habazi za uhakika ni kuwa Rivers United tayari wameondoka huko Nigeria na watawasili nchini wakati wowote kwa ajili ya mchezo dhidi ya Yanga

Wananchi hawapaswi kuingia kwenye mtego wa kuaminishwa kuwa Rivers United wamekubali kipigo na hivyo wanakuja kukamilisha ratiba tu

Jambo la uhakika ni kuwa mchezo wa Jumapili utakuwa mgumu, Yanga itapaswa kuchukulia kama ni mechi mpya pasipo kujali matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza

Habari njema ni kuwa baada ya ushindi wa Nigeria wachezaji na benchi la ufundi walitarajia hicho walichokifanya Rivers United. Wamefeli kwani watarajie kukutana na Yanga yenye njaa ya kutinga nusu fainali

Baada ya ushindi wa Nigeria, kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alibainisha kuwa bado hawajafuzu nusu fainali na kuwa ili kufanikisha hilo wanapaswa kushinda dhidi ya Rivers United baada ya mechi zote mbili

Mechi iliyopigwa Nigeria ni kama dakika 45 za kwanza na hii itakayopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili ni dakika 45 za pili

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top