SIMBA WANAIMANI NA MGUNDA

Uongozi wa Klabu ya Simba unamuunga mkono kocha Mkuu wa muda Juma Mgunda wakiridhishwa na kazi nzuri anayoifanya

Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema wanaridhishwa na kuimarika kwa timu chini ya Mgunda hivyo wanamuunga mkono kwa asilimia 100

"Mwalimu Mgunda anafanya vyema na ameonyesha uzoefu mkubwa alionao na sisi tupo nyuma yake, mpaka sasa hatuna shaka na uwezo wake," alisema Barbara

Mgunda amepewa jukumu la kuiongoza Simba katika michezo miwili muhimu ya ligi ya Mabingwa dhidi ya Primeiro De Agosto akianzia ugenini siku ya jumapili

Kama ataipeleka Simba hatua ya Makundi na pia akipata ushindi katika mchezo wa ligi ya NBC Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga Octoba 23, ni dhahiri Mgunda atakabidhiwa rasmi  majukumu ya kuwa kocha wa kudumu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post