Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wako tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa kesho jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Nabi amesema wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo huo katika mpango wao wa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi
Amesema wanakwenda kuchuana na Al Hilal ambao pia wana mahitaji kama yao hivyo utakuwa mchezo wenye upinzani mkali
"Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo huu unaotarajiwa kuwa mgumu. Wachezaji wako tayari, wanajiamini lakini pia wakiwaheshimu wapinzani wetu Al Hilal"
"Haitakuwa mechi rahisi kwa sababu ni mashindano makubwa na ifahamike mshindi wa kwenda hatua inayofuata ataamuliwa baada ya mchezo wa pili kule Sudan"
"Wachezaji wanafahamu hilo wana uzoefu wa michuano ya aina hii wanajua vile wanapaswa kucheza ili kuweza kupata matokeo mazuri nyumbani," alisema Nabi
Nae kiungo Gael Bigirima amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo kuwapa hamasa wachezaji
Gael amesema itakuwa mara yake ya kwanza kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika lakini wachezaji wengi wa Yanga wana uzoefu wa kushiriki michuano hiyo
Amesema wachezaji wako tayari na dhamira yao ni kupata ushindi ili kuwa na nafasi ya kutinga hatua ya makundi
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.