NIJUZE NIJUZE Author
Title: IWE JUA, IWE MVUA NI ZAMU YA SUDAN
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
KLABU ya Yanga imeshindwa kutamba katika uwanja wa nyumbani, Benjamin Mkapa baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Al Hilal ya Sudan mche...

KLABU ya Yanga imeshindwa kutamba katika uwanja wa nyumbani, Benjamin Mkapa baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Al Hilal ya Sudan mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkali, kwani Yanga ilianza kwa kasi kubwa dakika 15 za kwanza, lakini baadaye Al Hilal ikabadili mchezo na kuanza kuonyesha ushindani zaidi.

Mayele alianza kuifungia Yanga bao la kuongoza dakika ya 50 kwa shuti la umbali wa mita 20 baada ya kupokea pasi ya Khalid Aucho, ingawa pia alikosa bao la wazi dakika ya 58 baada ya kupokea pasi ya Morrison ambaye alipokea krosi ya Feisal Salum 'Fei Toto'.

Dakika 66 kocha wa Al Hilal alifanya mabadiliko ya kumtoa John Roubia na nafasi yake ikachukuliwa na Mohammed Yusuph, wakati huo Yanga ilimtoa Jesus Moloko akaingia Tuisila Kisinda na Morrison nafasi yake ikachukuliwa na Farid.

Yusuph alitumia dakika moja tu (dakika 67) kuisawazishia timu yake bao na kuufanya mlima mrefu kwa Yanga iliyokuwa inahitaji ushindi nyumbani, lakini kwa sasa itakuwa na kibarua kigumu cha kushinda ugenini.

Kipa wa Yanga, Djigui Diarra baada ya kuruhusu bao hilo dakika ya 67 alionekana kunyong'onyea na kukuchumaa chini kwa muda, ingawa aliisaidia zaidi timu dakika za mwishoni ambazo aliokoa hatari zaidi ya tatu ambazo isingekuwa umakini wake wapinzani wangepata mabao.

Kocha wa msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze alisema walitarajia kupata ushindi, lakini kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 yanawapa kazi ngumu, ingawa alijipa moyo kwamba watakwenda kupambana.

"Hatukutarajia matokeo haya, kwani tulitaka tushinde mechi ili tukapambane zaidi ugenini," alisema.

Timu zinatarajia kucheza mechi ya marudiano Oktoba 16 jijini Khartoum Sudan.

Kikosi cha Yanga kilichoanza; Diarra, Job, Bangala, Kibwana, Djuma, Aucho, Fei Toto, Morrison, Moloko, Azizi Ki na Mayele.

Benchi walikuepo, Mshery, Mwamnyeto, Lomalisa, Farid, Makambo, Bacca, Mauya, Sure Boy na Kisinda.

 


About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top