MATCHDAY: YANGA vs KMC | NBC PL

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo watashuka dimba la Benjamin Mkapa kuwakabili watoza ushuru wa Kinondoni KMC katika mchezo utakaopigwa saa moja usiku


 


Matokeo ya Ushindi kwa Yanga katika mchezo huo yatawashuhudia vijana wa Kocha Nasreddine Nabi wakipanda Kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC

Hata hivyo hautakuwa mchezo mwapesi kutokana na ushindani ambao KMC wanaonyesha kwenye ligi msimu huu

KMC inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 13 katika mechi nane walizocheza

Katika mchezo uliopita waliichapa Azam Fc mabao 2-1 pia wakipata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba Sc

Kwa Yanga ni mchezo muhimu kupata ushindi ili kurejesha morali ya ushindi baada ya kucheza mechi tatu pasipo kushinda

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post