TUPO TAYARI KUIKABILI AZAM FC - JUMA MGUNDA

 Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

 Akizungumza katika Mkutano na wanahabari, Mgunde amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa asilimia 100 dhamira yao ikiwa ni ushindi
 
Mgunda amesema wanaiheshimu Azam Fc kwani ni timu nzuri lakini watapambana ili kuhakikisha wanaweza kuibua na ushindi
 
"Maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam Fc yamekamilika, tunajua itakuwa mechi ngumu, tunaiheshimu Azam Fc ni timu nzuri lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho ili kupata alama zote tatu", alisema Mgunda
 
Simba watakuwa ugenini katika mchezo huo ambao umehamishwa kutoka uwanja wa Azam Complex kwenda uwanja wa Benjamin Mkapa ukitarajiwa kupigwa saa moja usiku

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post