WAWA MWAKA MMOJA ZAIDI SIMBA

BEKI wa kati wa Simba raia ya Ivory Coast, Pascal Wawa, ameandaliwa mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo.


Wawa ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, ameandaliwa mkataba mpya baada ya timu hiyo kuachana na Junior Lokosa Junior.

Mtu wa karibu na mchezaji huyo, ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Kwa sasa Simba wana mpango wa kumuongeza Wawa mkataba wa mwaka mmoja baada ya Junior Lokosa kuondoka na mkataba huo atasaini hivi karibuni.

“Simba wanavutiwa na Wawa ambaye amekuwa na pacha nzuri na Onyango (Pascal) ambaye amejiunga na timu hiyo msimu huu pia ukiangalia tangu atue amekuwa kikosi cha kwanza mara kwa mara".

Alipotafutwa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu simu yake iliita bila kupokelewa.


 

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post