Shirikisho la Mpira barani Africa CAF limemtangaza Mchezaji wa Simba SC Clatous Chama kuwa ndie mchezaji bora wa Wiki hii katika ligi ya Mabingwa Afrika inayoendelea katika hatua ya makundi.
Hii ni mara ya pili kwa Simba SC kutoa mchezaji bora wa wiki kwani awali mchezaji Luis Miquissone #KONDEBOY katika roundi ya 2.
Chama amekuwa mchezaji bora wa wiki katika mzunguko wa 5 wa ligi hiyo akiwashinda wachezaji Amir Sayoud (CR Belouizdad), Ricardo Goss (Mamelodi) na Ferjani Sassi (Zamalek).
Katika Ligi hiyo Simba imekuwa Bora sana kwani hadi sasa imeweza kuwa klabu ambayo imejikusanyia alama 13 ndani ya mechi 5 hii ni pamoja na klabu ya Mamelodi.
Wakati huohuo Simba na Wydad tu ndio timu ambazo zimeruhusu goli moja tu la kufungwa katika mechi 5 katika timu bora 16 za afrika kwa msimu wa 2020/21.
Simba ni timu pekee kutoka Afrika Mashariki na Kati kuingia katika Top Five katika ubora kati ya timu 16 bora. Mazembe na Vita ziko katika nafasi ya 13 na 14
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.