Mtanzania Yohana Mkomola anayeichezea timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys amefunguka kuhusiana na kupata dili la kwenda kuichezea club maarufu ya soka ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
"Habari hizo ni kweli nilienda Etoile du Sahel kufanya majaribio katika timu yao kwa wiki mbili lakini nilifanya kwa wiki moja na nusu tu nikapata majibu kuwa nimefuzu" amesema Mkomola.

"Walikuwa wananifatilia maana nilivyomaliza mechi na Congo meneja wangu akaniambia kuwa kuna barua imekuja natakiwa kwenda kufanya majaribio Etoile du Sahel ambapo nitajiunga na kikosi chao cha pili chini ya umri wa miaka 20" Yohana aliongeza

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV
Tags
SPORTS NEWS