RAIS MAGUFULI ATEUA MKUU MPYA WA MAJESHI TANZANIA

Inatokea IKULU Dar es salaam ambapo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya utauzi wa Mkuu mpya wa majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania kama inavyosomeka kwenye hii taarifa hapa chini.
Venance S. Mabeyo
Aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya Davis Mwamunyange ni Venance S. Mabeyo (Pichani hapo Juu) ambapo pamoja na kuteuliwa kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.

Jenerali Venance anachukua nafasi ya Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu ambapo kitu kingine cha kufahamu ni kwamba Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania, Meja Jenerali James Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance aliyeteuliwa kuwa mkuu wa majeshi.

Uteuzi huu unaanza mara moja ambapo tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadae.
Taarifa

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM

Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post