Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari Jumatano hii ofisini kwake wakati akitaja orodha ya pili ya watuhumiwa wa madawa hayo, Makonda amesema, "Ukitaja jina kwanza utakuwa unaingia kama vile unajitahidi kuhama".
"Hebu wewe kama una taarifa za mitandao sahihi tuambie tu, ndio maana nimesema tunapokea kwa wenyeviti wa mitaa, tunapokea wapi, wewe kama una taarifa sahihi wewe tuambie tu. Lakini usiibue taarifa kwa sababu wewe una jambo la kujibu ukaibua taarifa nyingine tena siyo rasmi, tena nimeeleza hapa ukiwa kwenye mahabusu au popote pale chini ya usimamizi hata simu huruhusiwi kuwa nayo," ameongeza.
"Kwahiyo bado vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kucheki pia utaratibu gani uliotumika kwa mtu kujirekodi na kuanza kutoa matangazo wakati upo sehemu sahihi ya kutoa hizo taarifa".
Majina 65 ya watuhumiwa wa wanaojihusisha na madawa ya kulevya yametajwa kwenye orodha ya awamu ya pili yakiwemo majina makubwa nchini Freeman Aikaely Mbowe, Yusuf Manji, Mchungaji Josephat Gwajima, Iddi Azan na Hussein Pambakali.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.