HII NDIO KAULI YA CHAMA CHA CHADEMA JUU YA KIONGOZI WAO KUTAJWA KWENYE ORODHA YA PILI YA MAKONDA

Chadema
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo February 8, 2017 ametangaza kuiachia orodha ya Watu 65 wanaotuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya ambapo amemtaja pia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ndani yake.

Dakika chache baada ya kumtaja, CHADEMA Makao makuu Dar es salaam walikutana na Waandishi wa habari na kusema yafuatayo.
“Kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani".

“Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita"

"Kitendo cha kwenda kuongea kwenye mkutano na Waandishi wa habari na kutaja viongozi wakuu wa kitaifa ambao wana tuhuma tu ambazo hazijathibitishwa, ni kukosa ustaarabu wa kiuongozi… tusingependa kuona viongozi wengine Waandamizi kutendewa kama alivyotendewa kiongozi wa chama chetu"

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post