Unknown Unknown Author
Title: MADIWANI MANISPAA YA LINDI WACHACHAMAA, WAIKATAA TAARIFA YATUME YA UCHUNGUZI MIRADI YA TASAF
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Lindi. Baraza la halmashauri ya manispa ya Lindi, jana walikataa kupokea taarifa ya tume iliyoundwa kuchunguza utekelezaji...
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Baraza la halmashauri ya manispa ya Lindi, jana walikataa kupokea taarifa ya tume iliyoundwa kuchunguza utekelezaji wa miradi iliyochini ya mfuko wa maendeleo ya jamii wa mpango wa kuondoa umasikini (TASAF) katika manispaa hiyo.
TASAF
Madiwani hao bila kujali tofauti za itikadi zao za kisiasa walikataa kupokea taarifa hiyo wakati kikao cha baraza la madiwani, ikiwa ni kikao cha pili cha robo ya mwaka wa fedha wa 2016/2017 kilichofanyika kwenye ukumbi wa maendeleo uliopo katika manispaa hiyo. Kwamadai kwamba tume hiyo ilichunguza eneo moja la ulipaji wa malipo kwa kaya masikini badala ya miradi yote kama ilivyoagizwa.

Walisema miradi mingi inayotekelezwa kupitia mpango huo inatia mashaka. Hivyo haikuwa sahihi kwa tume hiyo kuchunguza eneo moja wakati malalamiko yapo katika miradi mingi na maeneo mengi.

Diwani wa kata ya Mnazi mmoja, Said Mateva, alisema haikuwa sahihi tume hiyo kuacha kuchunguza miradi inayolalamikiwa kila mara na iliyo wazi. Badala yake imechunguza eneo moja tu kati ya mengi ambayo utekelezaji wake unatia mashaka.

Alitolea mfano kwenye kata yake kunafedha ziliendelea kulipwa kwa watu waliofariki na wasionavigezo vya kunufaika na mpango huo. Hata hivyo wahusika hawajachukuliwa hatua hadi sasa. Ingawa amekuwa akilieleza jambo hilo ndani na nje ya baraza hilo.
"Mara moja zilichukuliwa takribani shilingi lakimbili kwa ajili ya kununua mafuta, wakati thamani halisi ya malipo yake ni shilingi 52,000 tu, baada ya kupigwa kelele sana fedha hizo zilirejeshwa na kuingizwa kwenye akaunti za vikundi. Kuna vikundi vinne vilipewa semina siku moja ndani ya ukumbi mmoja, lakini wawezeshaji walijilipa posho ya siku nne, yote hayakuchunguzwa". 

Mateva aliutaja mradi mwingine unaotia mashaka ni kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone. Akibainisha kwamba hata njia zilizotumika kumpata mzabuni wa ujenzi wa tangi zinatia mashaka. Diwani wa kata ya Mitandi, Hafidh Kitutu alisema mpango wa serikali wa kuziondolea umasikini kaya zisizo na uwezo katika halmashauri hiyo hautafanikiwa iwapo hali itaendelea kuachwa bila kudhibitiwa.

Hivyo kunahaja ya kuundwa tume nyingine itakayochunguza miradi yote inayotiliwa mashaka na kulalamikiwa na wananchi. Maelezo ya madiwani hao yaliungwa mkono na diwani wa kata ya Mtanda, Abeid Bakari aliyewashauri madiwani wenzake wasipokee taarifa hiyo. Kwani licha ya kuwa na ya eneo moja, lakini pia hawakupewa mapema kabla ya kikao hicho iliwaisome. 

Ambapo diwani wa kata ya Ndolo, Issa Luono aliwaeleza madiwani wenzake wasiogope gharama wakubali kuunda tume nyingine na waachane na taarifa iliyokuwa mbele yao.
"Ukitaka kumpa talaka mke usiogope hasara wala gharama ulizotumia kwake, ukijuliza hayo huwezi kumuacha, utazidi kuumia, utaendelea kupata karaha na hasara. Tuunde tume nyingine wala hatumtafuti mtu bali tunatekeleza wajibu wetu kwa wananchi," alisema Luono.

Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa hiyo, Jomaary Satura licha ya kusema hakuwa na kipingamizi kuhusu kuundwa tume nyingine. Hata hivyo aliwatahadharisha na kuwaasa madiwani hao kwamba tume hizo zinatumia fedha za wananchi. Hivyo wasiunde kwa ajili ya kujinufaisha.

Alisema ni jambo la kushangaza kuona madiwani hao wanakataa kupokea taarifa wakati mwenyekiti wa kamati ya fedha, ambae pia ni makamo meya wa halmashauri hiyo alizungukia miradi yote wala hakukosoa taarifa hiyo.
"Nakamati ya fedha ni kubwa kuliko hizo tume zinazoundwa". Satura aliendelea kuwaasa madiwani hao kuangalia maudhui na athari za kuunda tume mara kwa mara na miradi wanayokwenda kukagua.

Hata hivyo maelezo ya mkurugenzi huyo na ya meya wa halmashauri hiyo, Mohamed Lihumbo aliyeshauri taarifa hiyo ipelekwe na kujadiliwa kwenye kamati ya fedha hayakubadili msimamo wa madiwani hao. Hivyo taarifa hiyo haikupokelewa na ilikubalika iundwe tume nyingine.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top