NIJUZE NIJUZE Author
Title: TUANZEBE AJITIA KITANZI NDANI YA MANCHESTER UNITED HADI 2020
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Kinda kutoka klabu ya Manchester United , Axel Tuanzebe , hatimae amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo, ikiwa ni siku k...
Kinda kutoka klabu ya Manchester United, Axel Tuanzebe, hatimae amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo, ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuchezeshwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha wakubwa.
Axel Tuanzebe
Tuanzebe mwenye umri wa miaka 19, alitumika kama mchezaji wa akiba wakati wa mchezo wa kombe la FA, ambapo Man Utd waliibuka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri dhidi ya Wigan mwishoni mwa juma lililopita.

Mkataba wa mchezaji huyo mzaliwa wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni wa miaka mitatu na utafikia kikomo mwaka 2020, huku taarifa za ndani ya klabu ya Man Utd zikieleza kuwa, huenda akaongozewa mkataba mwingine endapo ataendelea kufanya vizuri.

“Nilikua shabiki mkubwa wa Man Utd, lakini hii leo ni sehemu ya wachezaji wa klabu hii, ninafarijika sana.” Tuanzebe aliiambia tovuti ya Man Utd. “Kucheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha wakubwa tena kwenye uwanja wa Old Trafford ilikua sehemu ya ndoto zangu, naamini hata familia yangu imefurahi.

“Nimekua ninajifunza mambo mapya kila kukicha, ninapata ujuzu kutoka kwa wachezaji wenzangu, ninatarajia kupata mengi zaidi kutoka kwa wachezaji wa kikosi cha wakubwa ambao nimeshacheza nao mara moja katika mchezo wa kombe la FA mwishoni mwa juma lililopita.”

Tuanzebe alisajiliwa na Man Utd mwaka 2013 katika kituo cha kulea na kuwaendeleza vijana cha klabu hiyo, na amekua akionyesha juhudi za kupambana.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top