Unknown Unknown Author
Title: WAZAZI KILWA WAUNGA MKONO ADHABU YA VIBOKO MASHULENI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Kilwa. KATIKA kudhibiti ni dhamu ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari wilayani Kilwa mkoani Lindi. Baadhi y...
Na. Ahmad Mmow, Kilwa.
KATIKA kudhibiti ni dhamu ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari wilayani Kilwa mkoani Lindi. Baadhi ya wazazi wameunga mkono adhabu hiyo nakutoa wito iendelee. Bali sheria, kanuni na taratibu za utoaji wa adhibu hiyo zifuatwe.
Wanafunzi na Wazazi
{Picha kutoka Maktaba}
Wakizungumza kwenye semina ya wadau wa elimu iliyoandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania (TENMET) kwa kushirikia na wadau wengine, kuhusu uwasilishaji wa matokeo ya utafiti wa mradi wa uhamasishaji wa elimu bora kwa kutumia rasilimali za ndani wilayani humo.

Walisema ili kudhibiti nidhamu ya wanafunzi shuleni itayosababisha kupandisha kiwango cha ufaulu, kunahaja ya kuendelea kutumika. Hata hivyo utekelezaji wake usitumike vibaya na kusababisha ukatili dhidi ya wanafunzi.

Mzee Alli Mng'umba akizungumzia adhabu hiyo, alisema bado ni muhimu na inafaa kuendelea. Hata hivyo baadhi ya walimu wanaitumia vibaya na kugeuka ukatili dhidi ya wanafunzi. Kwamadai kuwa hawazingatii sheria, taratibu na kanuni katika kutumia.

Akibainisha kuwa iwapo walimu watazingatia mambo hayo hakutakuwa na matukio mengi ya walimu kutenda vitendo vya kikatili dhidi ya wanafunzi.
"Kuna tofauti kati ya fimbo na kiboko, hata hivyo baadhi ya walimu wanatumia fimbo badala ya viboko, kiboko ni laini na hakiwezi kumjeruhi mwanafunzi ingawa anasihisi maumivu, lakini fimbo zinawajeruhi kwasababu ni ngumu," alisema Mng'umba.

Mzazi huyo ambae pia ni mtunza hazina wa bodi ya mtandao wa asasi za kiraia za wilaya ya Kilwa (KINGONET), alisema baadhi ya walimu wanazidisha idadi ya viboko vinne iliyoruhusiwa kisheria na wanapiga sehemu yoyote ya viungo vya miili ya wanafunzi.

Lakini pia hawazingatii kanuni katika upigaji.
"Hawa angalii kwamba msichana anatakiwa apigwe akiwa amesimama, na mvulana akiwa amelala. Tena zamani ni walimu wakuu na wakuu wa shule tu ndio waliokuwa wanaruhusiwa kutoa adhabu hiyo, lakini sasa kila mwalimu anapiga tu," alisema Mng'umba.

Mwanakamati wa kamati ya shule ya msingi Mirumba, Arafa Mboma, licha ya kuunga mkono adhabu hiyo, alisema baadhi ya shule wajumbe wake wa kamati hawashirikishwi na kuambiwa idada ya viboko wanavyo sitahili kupigwa wanafunzi wanapofanya makosa.

Bali wanaambiwa na watoto wao kwamba walimu wamewaeleza kuwa idadi ya viboko wanavyositahili kupigwa ni vinne. Huku akisema baadhi ya walimu wanazidisha idadi hiyo na wanapiga sehemu yoyote.
"Sisemi kama iondolewe, kwasabubu ikiondolewa shuleni hakutakuwa na nidhamu tena bali vurugu na kiwango cha ufaulu kitazidi kushuka. Baadhi ya watoto wetu hawana nidhamu kabisa," alisema Arafa.

Nae mwenyekiti wa kamati ya shule ya Lihimalyao, Hassan Kikomo, alisema ingawa adhabu hiyo ni mzuri katika kudhibiti nidhamu ya wanafunzi, hata hivyo inakasoro ambazo zitasababisha wanafunzi wawaone baadhi ya walimu niwakatili na wengine ni wema.
"Hakuna sababu ya walimu wakuu peke yao kuwa na uwezo wa kutoa adhabu hiyo au kuwateua walimu fulani watoe adhabu hiyo, wote wanataaluma moja na wote niwalimu. Huko nikujenga matabaka yatayosababisha wanafunzi wawachukie baadhi ya walimu, jambo la msingi wote wazingatie taratibu, kanuni na sheria katika kutoa adhabu hiyo," alishauri Kikomo.

Kwa upande wake, mwasilishaji wa matokeo ya utafiti huo, Jacob Kateri, alisema kwa mujibu wa utafiti huo uliofanyika katika shule 15 za msingi zilizopo katika wilaya hiyo na kuwahoji baadhi ya wanafunzi, walimu wa kuu, walimu, wazazi, wajumbe wa kamati za shule na viongozi kwa kuzingatia modeli ya haki msingi 10 za kupata elimu bora. Ambapo haki sita zilijadiliwa wakati wa utafiti huo.

Alisema adhabu ya viboko imeripotiwa kuwepo kwa kiasi kikubwa katika shule 14 kati ya 15. Ambapo wahusika wakubwa waliotajwa zaidi katika kutumia adhabu za viboko ni walimu na wazazi.

Aidha mtafiti huyo kutoka shirika la ActionAid ambalo ni miongoni mwa wadau wa utekelezaji wa mradi na utafiti huo uliofanyika kuanzia mwezi Aprili hadi Mei mwaka huu na kuwasilishwa jana kwenye semina hiyo, alisema katika utafiti huo 67.7% ya walimu walibainika kuwa walipata mafunzo ya kuheshimu haki za watoto, huku 32.3% walikuwa hawajapata mafunzo.

Wadau wa utekelezaji wa mradi huo wa uhamasishaji wa elimu bora kwa kutumia rasilimali za ndani unaofadhiliwa na shirika la misaada la Norway (NORAD) ni ActionAid, TANMET, CWT kwa ngazi ya taifa, KINGONET na MEDO.

Shule zilizofanyiwa utafiti wilayani humo ni Masoko, Lihimalyao Kusini, Mavuji, Matanda, Mirumba, Kinjumbi, Migeregere, Kikanda, Somanga, Njinjo, Kibata, Nandembo, Chumo, Mingumbi na Namayuni.
********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top