Unknown Unknown Author
Title: SIMULIZI:: SITALIA TENA SEHEMU YA 06
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SIMULIZI:: SITALIA TENA SEHEMU YA 06 MTUNZI: NYEMO CHILONGANI ILIPOISHIA.....!!! Hakukuwa na mtu, watu wote wakiwemo polisi walikuwa wa...
SIMULIZI:: SITALIA TENA
SEHEMU YA 06
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
SIMULIZI:: SITALIA TENA SEHEMU YA 06
ILIPOISHIA.....!!!
Hakukuwa na mtu, watu wote wakiwemo polisi walikuwa wamekimbia. Walipotoka nje ya geti tu, harakaharaka Hassan na wenzake wakawafuata na kuwaambia waingie ndani ya gari. Wakaingia na kuanza kuondoka.

SONGA NAYO....
Watu walikimbia, hawakujua ni kitu gani kilichoendelea katika uwanja ule. Kila mmoja aliogopa na hakukuwa na mtu aliyekuwa tayari kuona akifa baada ya mwanamke huyo kutaka kujitoa mhanga.


Mabomu yale yaliwaogopesha, kila mmoja aliogopa, matukio kadhaa ya watu waliokuwa wakijitoa mhanga katika nchi za Waarabu yaliwaogopesha na walijua kwamba mabomu aliyojivika Yasmin yalikuwa ya kweli.


Wakakimbia na kuelekea mbali kabisa na uwanja ule, hawakujua ni kitu gani kiliendelea, hawakujua kama mwanamke huyo alikwenda pale kwa ajili ya kumuokoa Saida. Kule walipokuwa, masikio yao yalikuwa yakisikilizia milipuko ambayo ingesikika ndani ya uwanja huo, walisikilizia na kusikilizia lakini hakukuwa na kitu.


Baada ya ukimya wa saa moja, polisi wakaanza kurudi katika uwanja ule, walitaka kuona ni kitu gani kilikuwa kimetokea kwani hawakusikia mlipuko, walitaka kuona kama mwanamke yule alijilipua au nini kilitokea.


Walipofika huko, kitu cha ajabu kabisa, kilichowashangaza, hawakukuta mtu yeyote yule. Kila mmoja akabaki na mshangao, hakuwepo Saida wala mwanamke huyo na hivyo kujua kulikuwa na mchezo ulifanyika.


Hawakutaka kubaki kimya, walichokifanya ni kupiga simu katika vituo vingine vya polisi na kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea kwamba msichana aliyetakiwa kuuawa, hakuwepo, kulikuwa na mwanamke aliyefika mahali hapo na kumchukua.


“Alimchukuaje?” aliuliza polisi upande wa pili.
“Yaani alijifanya kuja hapa akiwa na mabomu...”
“Halafu?”
“Wote tukaogopa na kukimbia...”
“Halafu...”
“Tukahisi kwamba mabomu yangelipuka, baada ya kurudi, hatukukuta mtu,” alisema mwanaume huyo kwa njia ya simu.
“Kwa hiyo mkakimbia kuogopa mabomu?”
“Ndiyo mkuu...”
“Hivi kweli mnaogopa mabomu! Kweli tunakuwa na askari wanaoogopa mabomu!” alisikika mkuu huyo kwenye simu.


Hilo halikumuingia akilini, hakuamini kama kungekuwa na polisi ambao wangeogopa mabomu. Mabomu hayakuwa jambo la ajabu nchini Oman au katika nchi nyingine za uarabuni, huko, watu walifanya kila liwezekanalo kuyaokoa maisha ya watu lakini si kuogopa mabomu.


Haraka sana taarifa zikaanza kutolewa kila kona kwamba msichana Saida alikuwa ametoroshwa na watu wasiojulikana. 


Kwa msaada wa kituo cha polisi alichokuwa amefikishwa usiku uliopita, picha zake zikachapishwa na kuanza kusambazwa kila kona nchini Oman.

Taarifa za kutoroshwa kwake ziliwachanganya watu wengi, mashirika mengi ya habari ya televisheni za Kiarabu yakaanza kutangaza kile kilichotokea huku wakionyesha kwenye televisheni namna watu walivyokuwa wakikimbia kutoka ndani ya uwanja ule kwa ajili ya kuyaokoa maisha yao.


Hilo lilikuwa tukio ambalo liliwaacha watu midomo wazi. Hakukuwa na mtu aliyewahi kuukimbia mkono wa sheria, tena katika uwanja siku ya hukumu. Kila mtu aliwapa lawama polisi, ni kweli walijitetea kwamba kulikuwa na mwanamke aliyeingia ambaye alivaa mabomu lakini hawakujua mwanamke huyo alikuwa nani na alitumwa na nani.


“إغلاق الحدود لثمان وأربعين ساعة، لا يسمح لأحد من أن أي شخص سوف يحقق القبض,” (fungeni mipaka kwa saa arobaini na nane, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kutoka na yeyote ambaye atafanikisha kukamatwa kwa mwanamke huyu, atapewa zawadi nono) alisikika kamanda wa jeshi la polisi jijini Muscat.


Hakukuwa na muda wa kupoteza, haraka sana mipaka ikafungwa na watu kutakiwa kuwa makini njiani kuhakikisha mwanamke huyo anakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.


Barabarani, kila kona picha zake zilisambazwa, watu walimwangalia kwa hasira kali, wengi walipoiona sura yake, waliomba dua ili aweze kukamatwa kwani kwa kile alichokuwa amekifanya, kilikuwa kikubwa ambacho hakutakiwa kuonewa huruma kwa staili yoyote ile.


Baada ya saa mbili, polisi wakaona ni lazima wawasiliane na mzee Abdulaziz kwani walikuwa na hofu kwamba inawezekana kwa kutumia fedha zake mzee huyo akawa amehusika katika kumtorosha Saida.


Walichokifanya ni kuelekea nyumbani kwa huyo mzee, walipofika, wakakaribishwa na kuingia ndani. Wakataka kuonana naye hivyo kwenda kuitiwa. Walipomuona, wakamuweka kikao na kumwambia kile kilichotokea.


“لغرض المجيء إلى هنا هو,” (kwa hiyo lengo la kuja hapa ni nini?) aliuliza bwana Abdulaziz.
“....ونحن نرى أن كنت طرفا,” (tunahisi kwamba umehusika...)
“؟في ماذا,” (katika nini?)
“اختطاف,” (kumtorosha)
“ماذا في ذلك؟ ؟انها يا أخي ا (nimtoroshe ili iweje? Ni ndugu yangu? Ni mtoto wangu?) aliuliza huku akiwa amewakazia macho.
“لذلك نحن بحاجة الشرطة تساعدني على شيء واحد,” (basi tunahitaji uisaidie polisi juu ya kitu kimoja.)
“؟التماثيل (kipi?)
“مع العلم الذين مشربة (kumfahamu aliyempa mimba)
“اليوم الذي اكتشفت أنها حامل، قد يكون لنفسه يمكن قال لنفسه. إذا انه لم يجلس هنا من نهاية,” (Inawezekana alijipa mwenyewe. Kama alikaa humu ndani hakuwahi kutoka, mwisho wa siku akagundulika kwamba alikuwa na mimba, inawezekana alijipa mwenyewe) alisema mzee huyo, kwa jinsi alivyoonekana tu, alikuwa na hasira kali.


“شيخ... (mzee...)
“؟يمكنك ترك بيتي (mnaweza kuondoka nyumbani kwangu?) aliuliza mzee huyo.


Hawakuwa na jinsi, wakaondoka huku wakiwa na maswali mengi ya kumuuliza mzee huyo. Walikuwa na uhakika kwamba mzee huyo alihusika katika kumtorosha Saida, hawakumfikiria kabisa Kareem.


Walipofika kituoni, wakamwambia mkuu wa kituo kile kilichotokea, majibu ya dharau waliyopewa na mwanaume huyo. Mkuu wa kituo akawaamuru waondoke na kumkamata mzee huyo na kumpeleka kitioni.


Hilo likafanyika na baada ya nusu saa, mzee huyo alikuwa kituoni hapo. Hakutetemeka, alivyoonekana, alionekana kuwa na hasira, hakupenda kukamatwa kwake, alijijua jinsi alivyokuwa na fedha, alivyoheshimika kila kona Oman, kitendo kile kilionekana kama kumkosea heshima.


“Nikusaidie nini?” aliuliza mzee huyo huku akimwangalia mkuu wa kituo.
“Ninahitaji kujua ukweli!”
“Kuhusu nini?”
“Aliyempa mimba huyu mwanamke!”
“Niliwaambia wenzako kwamba inawezakana alijipa mwenyewe...” alijibu tena kidharau.
“Unamaanisha nini?”
“Kama alikuwa ndani tu siku zote, hakuwahi kutoka, ghafla akapata mimba, nani alikuwa amempa?” aliuliza mzee huyo.


Hakukuwa na swali alilojibu kama ilivyotakiwa, walimuhoji kwa saa moja, majibu yake yalikuwa yaleyale yaliyojaa dharau kiasi kwamba kila mmoja ndani ya ofisi hiyo akaonekana kukasirika.


Wakati mahojiano yakiendelea, polisi wengine walikuwa wakiwasiliana kwa simu na polisi wengine. Waliendelea kupata taarifa kutoka mitaani, wanawake wote ambao walihisiwa kwamba wanaweza kuwa Saida walisimamishwa na kuamriwa wavue nikabu, walipofanya hivyo na kuonekana si wao, wakaruhusiwa waondoke.


Baada ya saa mbili, simu ikapigwa makao makuu. Harakaharaka kamanda mkuu akaichukua na kuipeleka sikioni kwani muda huo simu ilikuwa kitu muhimu kuliko kingine.
“Kuna nini?”
“Tumelipata gari alilokuwa huyo mwanamke!”
“Mwanamke yupi? Mwenye mabomu au Saida?”
“Wote wawili! Wapo kwenye gari ambalo tunalifuatilia sasa hivi...”
“Wapi?”
“Huku Qarn Al Alam.”
“Hakikisheni mnawakamata. Nawaongezea polisi huko!”
“Sawa mkuu! Tupe dakika thelathini, watakuwa mikononi mwetu wote wawili,” alisikika mwanaume kutoka upande wa pili. Simu ikakatwa. Kamanda akashusha pumzi nzito.

Je, nini kitaendelea? Usikose Kuungana nasi Saa Moja Asubuhi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top