NEDY MUSIC AGOMA KUFANYA KAZI NA WCB WASAFI

Hit maker wa ngoma ya “Usiende mbali” na Msanii kutoka lebo ya PKP Nedy Music, ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ya “Rudi” iliyotoka hivi karibuni akiwa na Christian Bella.
Nedy Music
Nedy Music, ameweka wazi kuwa hajafanya collabo yoyote na msanii kutoka lebo ya Wasafi na wala hajafikiria kufanya hivyo kinyume na taarifa ambazo zinaenezwa na watu kuhusu suala la kufanyika kwa Collabo hiyo.

Nedy ametoa msimamo huo bila kueleza kwa kina sababu ya maamuzi hayo, alipokuwa katika kipindi cha FNL cha EATV.


Nedy ambaye ametoa ngoma yake ya pili chini ya PKP aliyo mshirikisha Bosi wake Ommy Dimpoz, amesema taarifa hizo siyo za kweli na kwamba hana ugomvi wowote na Wasafi, isipokuwa kinacho endelea ni masuala ya kazi tu.

Kuhusu yeye kusalimiana na Wasafi amesema hana kinyongo na akikutana nao mahali popote atawasalimia
“Nikikutana na Msafi (msanii kutoka Wasafi) yoyote nitamsalimia kama kawaida kama washkaji, lakini kama yeye hataonesha ushirikiano basi salamu itakuwa haina haja”



**********************

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post