DC MWANZIVA AONGOZA KIKAO CHA MAPOKEZI YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva ameongoza kikao Cha Maandilizi ya mapokezi ya mbio za mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mwaka 2025.

Akiongea na wajumbe wa kikao hicho kilichofanyika Machi 19, 2025 katika uwanja Ilulu DC, Mwanziva amesisitiza Ushirikishwajwi wa Wananchi pamoja na makundi mbalimbali Kwenye Jamii kuhusiana na masuala ya mwenge. 

Aidha DC Mwanziva ametoa maelekezo kwa watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanasimamia vizuri fedha za michango ya mwenge kutoka Kwa wadau na kuzifikisha sehemu husika.

Naye Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mhe. Frank Magali amewapongeza wajumbe wa kikao hicho Kwa kujitokeza kwa wingi kwenye kikao hicho muhimu ambacho kimetumika katika kujadili na kuleta mwanga kuelekea mapokezi ya mbio za mwenge, lakini pia amewaomba wajumbe hao kuendelea kujitokeza katika vikao vijavyo.

Akisoma taarifa ya miradi pendekezwa ambayo itapitiwa na mbio za mwenge wa Uhuru Kwa mwaka huu, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Dkt. Stanford Mwakatage amesema miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi shule ya Msingi Stadium wenye thamani ya shilingi 334,600,000.00, Ujenzi wa kituo Cha mafuta Cha Buti la Zungu kilichopo Ngongo chenye thamani ya shilingi 2,230,000,000.00, kuweka jiwe la msingi mradi wa Maji Runyu kitomanga.

Miradi mingine ni kuweka jiwe la msingi jengo la NHIF kata ya Rasbura wenye  thamani ya shilingi 60,737,000.00. kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa bara bara kwa kiwango cha lami kuelekea shule ya Sekondari Lindi Wasichana kata ya Kilangala wenye thamani ya shilingi 1,390,525,885.00. Mradi wa kikundi Cha mapambo (Salumu Decoration) kilichopo fisi wenye thamani ya shilingi 20,000,000.00 mapato ya ndani. Kutembelea kikundi cha uhifadhi na utunzaji wa mazingira shule ya Msingi Mnazi Mmoja 'B' pamoja na Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi kata ya Rasbura.

Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi inategemea kupokea mbio za Mwenge wa Uhuru kutoka Halmashauri ya Mtama Mei 27, 2025. Kauli mbiu ya mwenge wa Uhuru mwaka 2025 inasema:
"Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na Utulivu"

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post