WATAFITI WA TARI NALIENDELE WATAKIWA KUJIELEKEZA KWENYE MAZAO MENGINE MBALI NA KOROSHO NA UFUTA!

Na. Mwandishi Wetu. Mtwara
Watafiti na waataalamu kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo  (Tari Naliendele) mkoani  Mtwara wametakiwa waende kusimamia mazao mengine kama mpunga,mazao ya mbogamboga na mahindi ili kuinua uchumi wa Wanamtwara.

Akizungumza na wafanya kazi wa taasisi hiyo Mei 13, 2025 mkuu wa wilaya ya Mvomero  Judithi Nguli mgeni rasmi na mtoa mada kwenye kikao hicho cha mafunzo ya maadili  ya uma kwa wafanyakazi wa Kituo cha utafiti na Kilimo Tari Naliendele.


Nguli amesema ukishaisha msimu wa Ufuta na Korosho Mtwara inakuwa kimya sasa nendeni  mkasimamie na mazao kama mpunga, karanga na mazao ya mbogamboga ili kukuza uchumi wa Wanamtwara.

"Mkoa wa Mtwara unazalisha zaidi korosho muendelee kuilinda hiyo lakini msimamie na mazao mengine ili kuongeza uchumi wa wanamtwara; uchumi uzunguke watu watafanya biashara kama inavyo kuwa katika wakati wa ufuta. Kama watazalisha na mazao yachakula pesa haita toka nje ya Mtwara kwaajili ya kwenda kununua chakula sehemu nyingine"amesema Nguli

Nguli ameongeza kwakusema Naliendele inafursa ya ardhi  kwahiyo mradi wa zaidi ya korosho ambao upo kwenye tafiti uendelee.

"Mtwara kuna fursa ya ardhi  nimeambiwa mnaanza na tatafiti nawaombea muendelee nao wananchi wanahitaji muongozo wakitaalamu, Hakuna mwananchi mvivu kwenye pesa akiona waliopo shambani wamewezeshwa wakafanikiwa wakapata maendeleo hakuna atakae bakia nyumbani" amesema Nguli.

Nguli amewataka wataalamu hao wafanye kazi kwakufata maadili ya utumishi wa uma kwani unaweza ukawa na elimu kubwa tena mzuri lakini kama faili lako lina makando kando maadili yako hayako sawa huwezi kupanda cheo.

"Unaweza kuwa  na elimu mzuri lakini maadili yako yasiwe sawa huwezi kusogea sasa twendeni tukaweke mafaili yetu vizuri twendeni tukawatumikie wanamtwara  ukiwa na cv mzuri watakuona utasogea sehemu nyingine hata kama isiwe hapa Tari"
amesema Nguli mgeni rasmi na mtoa mada kwenye kikao cha maadili kwa wafanyakazi wa Tari naliendele.

Naye mkurungenzi wa kituo cha utafiti wa Kilimo Tari Naliendele Geradina Mzena  amesema kutokana na kuimarika kwa soko la Korosho, Karanga na Ufuta wameamua kuja na programu ya utafiti katika mazao ya Mpunga, Mahindi na mbongamboga.

"Kutokana na kuimarika kwa mazao ya korosho, mbaazi na ufuta tumeona wakulima wakipata pesa nyingi lakini inaishia kwenye kununua chakula tumeamua kuja na utafiti tutaanza na  mazao matatu ambayo ni mpunga,mahindi na mbogamboga tutatafuta mbegu bora zitakazo stawi vizuri kwa Lindi na Mtwara baada ya hapo tutafanya utafiti wa udogo kujua ni udongo gani utafanya vizuri  ili wakulima waje walime kwa tija. Sasa ili tufanikiwe ni lazima watumishi wawe na maadili ndiyo maana leo tumekuja na haya mafunzo"
amesema Mzena mkurugenzi wa kituo cha utafiti wakilimo Tari Naliendele.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya maadili ya uma wamesema mafunzo hayo yamewakumbusha kuwa na maadili mema katika kufanya kazi zao za utafiti.

Rahimu Menya afisa mfawidhi kituo kidogo cha Nachingwea amesema mafunzo hayo ya maadili ya umma yamewasaidia kuwakumbusha kuwa na maadili mema katika kufanya kazi zao za kila siku za utafiti na zitaenda kuwainua wakulima na wataenda kupata tija.

Yunisi Kachundwa mtaalamu kutoka Tari Naliendele kituo kidogo cha Manyoni amesema wamejifunza vitu vingi katika nyanja ya utumishi wa uma anaamini yataenda kuwasaidia katika utumishi wao.

"Elimu tumeipokea vizuri  sana tunejifunza vitu vingi na vitaenda kutusaidia katika kazi zetu za kila siku, Mafunzo haya tulikuwa tunayahitaji leo tumejua ni namna gani utumishi wetu unafaida katika jamii yetu" amesema Kachundwa mtaalamu kutoka Tari Naliendele kituo kidogo cha Manyoni.

Kwaupande wake mkurugenzi mkuu wa utafiti wa kilimo Tari Dk Thomasi Bwana akizungumza kwa njia ya mtandao  amesema kwasababu viongozi wengi ni watafiti na wengine wanawatoa maabara na kuwapa nafasi ya kuongoza ndiyo maana wametaka wawapige msasa.

"Katika vituo vyetu kwa viongozi kimsingi ni watafiti lakini tunawachukuwa waje wasimamie rasilimali watu na pesa na rasilimali zingine sasa tumeona unaweza kumlaumu mtu kumbe alichokuwa anakifanya hakijui ndiyo maana tumekuomba uje uwapige msasa.Tari  inahitaji rasilimali aridhi ili tuweze kulima mashamba yetu pia kuweka miundombinu ya kilimo". amesema Mkurugenzi mkuu Dk Bwana.

Pia Dk Bwana amesema majukumu ya Tari ni pamoja na kufanya tafiti na kuchukuwa tecknolojia na kuzipeleka kwa wakulima ili kuzifanyia kazi.

"Majukumu ya Tari ni kufanya tafiti na kuchukuwa tecknolojia na kuzipeleka kwa wakulima ili waweze kufanya kazi pamoja na kutoa ushauri kwa viongozi wetu ili mkienda kutoa sera na kusimamia kazi muweze kuwa na ushaidi wa kisayansi." amesema Dk Bwana

Dk Bwana ameongeza kwakusema "Kwasasa tunawafanyakazi takribani 1000 na wote wanatumia aridhi na rasilimali za serikali katika vituo vyetu, Kimsingi  viongozi wetu mi watafiti na tunawachukuwa waje wasimamie rasilimali watu pesa na rasilimali zingine.amesema Dk Bwana mkurungenzi mkuu Tari.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post