Unknown Unknown Author
Title: LULU DIVA AFICHUA UKWELI JUU YA KULALA NA BARNABA CLASSIC
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwanadada ambaye ameingia kwa kasi ya aina yake kwenye game ya Muziku wa Bongo fleva, Lulu Diva , amevunja ukimya na kufunguka kuhusu ske...
Mwanadada ambaye ameingia kwa kasi ya aina yake kwenye game ya Muziku wa Bongo fleva, Lulu Diva, amevunja ukimya na kufunguka kuhusu skendo ya yeye kulala chumba kimoja na msanii Barnaba Classic, walipo kuwa wamekwenda kufanya video nchini Afrika Kusini.
Lulu Diva
Akifunguka kwa watanzania, Lulu amesema taarifa hizo siyo za kweli na kwamba anamchukulia Barnaba kama kaka yake, hivyo hawezi kumvunjia heshima kwa kuwa na mahusiano naye, wakati akijua kuwa Barnaba anaye mkewake wa ndoa.

“Barnaba na mimi tunaheshimiana sana, tulipokwenda Sauzi hatukufanya chochote, yule ni kaka yangu hata tukiwa chumba kimoja hatuwezi kabisa kufanya chochote, yule ni kaka yangu, kwahiyo taarifa hizo siyo za kweli” Alisema Lulu kwenye FNL.

Kuhusiana na mahusiano yake na mke wa Barnaba amesema wanafahamiana na wanaishi kama marafiki,

“Mimi na mke wake tunafahamiana na ni marafiki wa karibu sana na mambo mengine tunashauriana”.
Lulu Diva na Barnaba
Amesema kila kitu walicho kifanya kule kilikuwa ni sehemu ya kazi iliyowapeleka kule na si vinginevyo.

Mbali na Barnaba, Lulu alipangua pia skendo nyingine zinazomkabili za kutoka kimapenzi na wasanii wa kiume Bongo, na wote alisema ni kaka zake.

Lulu amefanya kolabo na Barnaba na tayari ameachia video ya ngoma hiyo inayokwenda kwa jina la Milele ambayo ndani ya wiki mbili ilikuwa imefikisha views zaidi ya laki 2.

__________________________________________
  • MFAHAMU VIZURI ZARI WA DIAMOND PLATNUMZ

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top