Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema.
Na,Vero Ignatus.Arusha.
Kesi iliyokuwa isikilizwe leo 22 disemba 2016 inayomkabili mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema ya kumtukana mkuu wa mkoa Mrisho Gambo imeahirishwa kutokana na hali ya lema kuwa mbaya gerezani.
Taarifa za Lema kushindwa kufika mahakamani zimetolewa na wakili wa serikali Elizabeth Swai leo asubuhi kwa hakimu mfawidhi katika mahakama ya hakimu mkazi Augustino Rwezile, alisema alipata taarifa kutoka kwa Afisa Magereza mshatakiwa kwanza anaumwa hivyo siku ya leo alipewa mapumziko pamoja na hayo taarifa hizo hazijaeleza kwa undani ni tatizo gani linamsumbua mbunge huyo.
Pia alisema alipewa cheti cha mgonjwa cha zahanati ambacho kilionyesha mahudhurio ya mgonjwa kwenye zahanati hiyo kutokana na kuwepo na taarifa za kuumwa za mbunge huyo na kushindwa kufika mahakamani, aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine.
Leo ilikuwa ni siku ya kusomewa hoja za awali kwa mbunge huyo na mkwewe Neema Lema, ambapo pia shahidi wa kwanza kutoka jamhuri alikuwa George Katabazi alikuwa anatoa ushahidi.
Hata hivyo hakimu mfawidhi Augustino Rwezile amesema kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 18 januari 2017
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema wanakabiliwa na kesi ya kumtukana na mkuu wa mkoa Mrisho Gambo.
__________________________________________
- KIMENUKA...!! QUEEN DARLEEN NA ALIKIBA KUHUSU NGOMA YA "WAJUA"
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.