ALIKIBA ASHINDA TUZO YA SOUNDCITY MVP 2016

Majina ya washindi wa tuzo za Soundcity MVP 2016 yametangazwa kwenye ukumbi wa Eko Hotel jijini Lagos, Alhamisi hii. Jumla ya washindi 14 walitajwa kati ya washiriki 109 waliokuwa wakiwania tuzo hizo hapo mwanzo.
Soundcity MVP 2016
Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na wasanii wanne akiwemo Diamond, Vanessa Mdee, Alikiba na Navy Kenzo.


Kati ya hao wote ni Alikiba pekee aliyefanikiwa kuibuka mshindi na kupata tuzo hiyo ya VIDEO OF THE YEAR kupitia wimbo wake wa Aje.

Sauti Sol wamefanikiwa kushinda tuzo ya BEST GROUP huku Wizkid alifanikiwa kuibuka na tuzo kubwa ya AFRICAN ARTIST OF THE YEAR ambayo Diamond alikuwepo kwenye kipengele hicho.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post