Diamond Platnumz amekuwa na mwaka mzuri sana kwani karibia nyimbo zake zote alizotoa kwa mwaka huu zimeweza kupokelewa vizuri sana mbali tu ya kupokelewa vizuri lakini pia amekwara tuzo kibao kupitia kazi zake.
Mwezi uliopita kituo maarufu cha Radio nchini Australia cha RADIO AFRO AUSTRALIA kiliandaa tuzo za kutafuta nyimbo zilizofanya vizuri kwenye mabara tofauti tofauti na kwenye kipengele cha wasanii waliongiza nyimbo kutoka Bara la Afrika ni Diamond Platnumz kupitia wimbo wake wa Kidogo aliowashirikisha P Square kutoka Nigeria.
Sasa Good News ni kwamba wimbo huo umefanikiwa kuchukua Tuzo ya wimbo bora kwa mwaka 2016 huko Australia.

Sasa Good News ni kwamba wimbo huo umefanikiwa kuchukua Tuzo ya wimbo bora kwa mwaka 2016 huko Australia.
Kupitia mtandao wa Twitter kituo hicho cha Radio kimeandika "#1 radioAFRO Australia Song of the Year 2016 with @djiz @diamondplatnumz @rudeboypsquare @PeterPsquare #kidogo"
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV
Tags
HABARI ZA WASANII