AKOTHEE AWAPA MAKAVU LIVE MABLOGA WA KENYA

Msanii Mrembo kutoka kenya Akothee amewajia juu Mabloga wa Kenya kwa kile wanachoandika kuwa aliudanganya umma kuwa ujauzito wake umeharibika ili apate kiki ya kusikika zaidi kwenye Media.
Akothee
Ujauzito huo wa mapacha ambao uliharibika Tangu mwezi Agosti 2016 bado umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kiasi kwamba mrembo huyo ambae ninaweza kusema ni msanii wa kike tajiri zaidi Nchini Kenya, kuchukua uamuzi wa kulizungumzia suala hilo mbele ya Media.

Wiki iliyopita Kupitia kipindi cha Mambo mseto kinachorushwa na Citizen Radio ya Nchini humo alisema
Akothee
“Mwanzo kabisa nashangaa eti Akothee kupata ujauzito inakuwa ni bonge la ‘headline’ wakati vitu hivi ni vya kawaida sana. Kuna madai kuwa nilikuwa natengeneza kiki kwa ujauzito wangu uliotoka, jambo ambalo naliona kuwa la kipuuzi sana. Nina watoto watano tayari, sio kwamba mimi tasa, sasa msingi wa mimi kutengeneza kiki ya dizaini hiyo ni nini eti?” Alimaliza kwa kuuliza Mrembo huyo.
********** 

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post