Unknown Unknown Author
Title: WALIMU KILWA WALALAMIKA KIASI KIDOGO CHA RUZUKU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Kilwa. SERA ya utoaji elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari za umma kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha...
Na. Ahmad Mmow, Kilwa.
SERA ya utoaji elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari za umma kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, imetajwa kuwa nachangamoto nyingi zinazohitaji kutatuliwa ili iweze kutekelezeka nakutoa matokeo mazuri.
(Picha Kutoka Maktaba)
Hayo yameelezwa jana na baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule za msingi zilizopo katika wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi. 

Wakizungumza kwenye semina ya wadau wa elimu wakati wa uwasilishaji wa matokeo ya utafiti wa mradi uhamasishaji wa utoaji elimu bora kwa kutumia rasilimali za ndani, iliyofanyika mjini Kilwa Masoko.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mingumbi, Mohamedi Njaule, licha ya kuipongeza serikali kwa juhudi kubwa ya kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya elimu. Ikiwamo kutatua tatizo la uhaba wa madawati na nyingine nyingi, alisema sera ya kutoa elimu bure itaweza kupandisha kiwango cha ufaulu iwapo baadhi ya changamoto kuhusiana na sera hiyo zitaondolewa.

Mwalimu Njaule alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kiasi kidogo cha fedha za ruzuku kinachopelekwa shuleni ambacho hakitoshi kutekelezea malengo yanayokusudiwa kufanyiwa. Mwalimu huyo alitolea mfano kiasi cha pesa kinachopewa shule yake kuwa ni shilingi 264000 kila mwezi.

Kiasi ambacho hakikidhi kutekeleza mahitaji yaliyoainishwa. "Kiasi hichoshilingi 52000 sawa na aslimia 20 zinazotakiwa kutumika kwa ajili ya mitihani, lakini kwa shule kama yangu kwa mtihani mmoja zinahitajika walau 600,000.00 sasa kiasi kama hicho tunakigawanyaje, nashauri hiyo shilingi 10,000.00 ziende moja kwa moja kwa nwanafunzi na sio hiyohiyo kutumika kwenye vitabu," alisema Njaule.

Hata hivyo mwalimu huyo ambae alitoa wito kwa serikali kutoa ruzuku kwa uuwiano mzuri kulingana na mahitaji. Alisema sera ya elimu bila malipo imesababisha kiwango cha utoro kwa wanafunzi kupungua na uandikishaji wanafunzi umeongezeka.
"Hata kiwango cha ufaulu kimeongezeka, na hata watoto wasiojua kusoma nakuandika wamepungua, hayo yametokana na sera hiyo, nijambo jema sana," alisema Njaule.

Pia alitoa wito kwa kila mmoja anaeielewa tafsiri sahihi ya sera hiyo atimize wajibu wake kutoa elimu kwa jamii ili sera hiyo ieleweke. Kwasababu wananchi wengi wameacha kutimiza wajibu wao kwa watoto wao kwamadai kuwa serikali itafanya mambo yote.

Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Lihimalyao, Ahmad Chumu, alitoa wito kwa serikali iwashirikishe walimu wenyewe kwa kwenda kuchukua mawazo yao. Alisema wenye wajibu wa kuchukua maoni yao hawaendi shuleni, badala yake mambo mengi yanatengenezwa bila kuwashirikisha.
"Idha wasinidal amru fantadhiru saa (ukitegemeza jambo kwa mtu asiye sitahiki subiri matatizo)," alisema kwa lugha ya kiarabu na kutafsiri kwa kiswahili.

Alibainisha kuwa matokeo ya kutowashirikisha ni kama hayo yakupelekwa ruzuku isiyolingana na mahitaji. Shukuru Abdalla, mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chumo, alisema mpango huo ni mzuri sana, bali unahitaji kufanyiwa maboresho ili uweze kuwa na matokeo chanya zaidi.

Akitaja maeneo yanayositahili kuongezwa ni uboreshaji wa miundo mbinu,ikiwao vyoo. Kwa madai kwamba kwenye ruzuku inayotolewa, hakuna kipengele cha ukarababati wa miundo mbinu. Kuhusu fedha zinazotolewa kutokidhi nahitaji, mwalimu huyo alisema
"Daima fedha huwa hazitoshi katika maisha yetu yote, ni natural (asili) ya fedha, hakuna haja ya kulaumu fedha ni kidogo bali kila mmoja atimize wajibu wake. Maana hata tukikokotoa mishahara na posho zetu tutasema hazilingani na mahitaji yetu," Alisema Abdallah.

Mwanafunzi Seifu Bashiru wa shule ya msingi Kikanda, alisema wazazi wengi baada ya kusikia serikali inatoa elimu bure, hawataki kutimiza wajibu wao wakuwanunulia mahitaji muhimu ya shule.
"Waombwa wanasema walimu ni wezi kwasababu serikali inatoa fedha zote za mahitaji ya wanafunzi bali walimu wanaiba, wazazi wamekuwa wakali sana wanapoombwa na watoto wao," alisema Seifu.

Semina hiyo iliandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwamo mtandao wa mashirika yasio ya kiserikali katika wilaya ya Kilwa (KINGONET) na ActionAid kwa ufadhili wa shirika la misaada la Norway(NORAD).

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top