Unknown Unknown Author
Title: WANAFUNZI WAKUMBWA NA UGONJWA WA KUANGUKA, SHULE YA MSINGI NDITI-NACHINGWEA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea. Wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Nditi, wilaya ya Nachingwea, juzi walikumbwa na taharuki shuleni hapo...
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
Wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Nditi, wilaya ya Nachingwea, juzi walikumbwa na taharuki shuleni hapo. Baada ya wanafunzi 12 kuanguka na baadhi yao kupoteza fahamu.
wanafunzi kuanguka
Picha kutoka Maktaba (sio ya shule husika)
Wanafunzi hao ambao wote ni wasichana walikuwa wakianguka kwa nyakati tofauti. Kutokana na sintofahamu na tahauruki hiyo, mwalimu kiongozi wa shule hiyo, Amon Livigha alilazimika kusimamisha muda shuguli zote shuleni hapo kwa muda nakuruhusu wanafunzi wote warejee majumbani kwa wazazi wao.

Akizungumza na Lindiyetu.com kuhusu tukiohilo, mwalimu mkuu huyo alisema wanafunzi hao walianza kupatwa na mkasa huo tangu saa mbili asubuhi hadi saa tano asubuhi.

Wakati yeye akiwa darasani anafundisha."Nilipata taarifa nikiwa darasani nikiendelea kufundisha,watoto 12 walianguka siku hiyo.Hata hivyo wote hali zao ni mzuri na wanaendelea na masomo," alisema Livigha.

Mwalimu mkuu huyo alisema baada ya kuona hali hiyo alimjulisha na kumuomba idhini ofisa elimu wa wilaya ya Nachingwea wa shule za msingi (DEO), Kwasa Bulenga amruhusu asimamishe shugulizi zote hapo shuleni kwa muda wa saa walau moja, ili kupisha taharuki iliyokuwa inaendelea shuleni hapo.
"Kila baada ya muda mfupi wanafunzi walikuwa wanaanguka, ingawa ni siku moja tu lakini walianguka watoto 12. Namshukuru mkuu wangu wa idara alikubali ombi langu, niliwaruhusu waende nyumbani na baadae siku hiyo hiyo mchana walirudi," aliongeza kusema mwalimu Livigha.

Mmoja wa wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo, Melkizedik Makota, alisema akiwa kazini kwenye ghala la chama cha msingi cha ushirika cha Nditi ambalo lipo jirani na shule hiyo. Aliwaona baadhi ya watoto walioanguka wakiwa wamechukuliwa na wazazi wao wakisaidiwa na wanafunzi wenzao na walimu wakipelekwa majumbani kwao.

Bwana Makota alikiri kwamba hiyo ni mara ya kwanza kutokea kijijini hapo watoto kuanguka kwa wingi huo.

Akibainisha imewahi kutokea kwa watoto wachache wenye mapepo ambao wanafahamika. Lakini sio kama ilivyotokea siku hiyo. 

Mtendaji wa kata ya Nditi, Juma Mng'anga alikiri pia kutokea tukio hilo. Nakwamba kwa walitoa taarifa wilayani kwa msaada.
"Kizuri zaidi hao watoto wote wanaendelea vizuri na wanaendelea na masomo. Hata hivyo kamati ya shule, serikali ya kijiji na wazazi walikutana na kujadili suala hilo," alisema Mng'anga.

Nae muuguzi kiongozi wa zahanati ya Nditi, Awetu Omari, licha ya kusema hakuna mwanafunzi aliyepelekwa kwenye zahanati hiyo kwasababu ya tatizo hilo, alisema alisikia na kuwaona baadhi ya wazazi wakiwasindikiza majumbani watoto waliofikwa na mkasa huo.

Awetu alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kuwakimbizia wagonjwa majumbani. Akibainisha kuwa watalamu wa afya wapo kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali ambako wanaweza kupata misaada ya kitaalamu na ushauri.

Akizungumza kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea. Ofisa elimu wa shule za msingi wa wilaya hiyo, Kwasa Bulenga, alikiri kupokea taarifa hiyo kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nditi.

Nakwamba yeye, maofisa wenzake wa idara ya elimu na wataalamu wa idara ya afya wamepanga kwenda kwenye shule hiyo haraka.
"Nikweli nipigiwa simu na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nditi nakunijulisha tatizo hilo,nilimruhusu asimamishe shuguli za hapo shuleni kwa muda mfupi.Kesho tutakwenda huko na wataalamu wa afya," alisisitiza Bulenga.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top