Unknown Unknown Author
Title: LIWOPAC KUFIKISHA ELIMU KWA WATU 87427
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea. Katika kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa mpana kuhusu haki za msingi za binadamu, hasa za wanawake na wat...
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
Katika kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa mpana kuhusu haki za msingi za binadamu, hasa za wanawake na watoto. Shirika la kiraia la msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto katika mkoa wa Lindi (LIWOPAC) limedhamiria kufikisha elimu kwa watu 87,427 katika mkoa huu katika kipindi cha miaka minne.
LIWOPAC
Hayo yalielezwa mwanzoni mwa wiki hii na ofisa tathimini na ufuatiliaji wa miradi wa shirika hilo, Nelson Choaji, alipozungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa uboreshaji upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria katika wilaya ya Nachingwea, uliofanyika mjini Nachingwea.

Choaji ambae alizungumza kwaniaba ya mratibu wa mradi huo, Pius Phinias, alisema mradi huo unaofadhiliwa na shirika la uwezeshaji huduma za kisheria (LFS) ni mwendelezo wa mradi wa kwanza ulioanza mwaka 2013 na kumalizika kwa mafanikio makubwa mwaka jana.

Ofisa tathimini na ufuatialiaji huyo alisema awamu ya kwanza ilikuwa na mafanikio katika maeneo mbalimbali yaliyokusudiwa kufanyika.

Ikiwamo uanzishwaji wa vitengo vya wasaidizi wa kisheria katika kila wilaya.
"Lengo kuu la mradi katika awamu ya kwanza lilikuwa ni kusogeza huduma za msaada wa huduma za kisheria karibu na jamii hasa ya tabaka la chini.
Mafunzo ya sheria mbalimbali, ikiwamo ardhi, ndoa, mirathi na sheria juu ya haki za binadamu na haki za msingi hasa za wanawake na watoto yalitolewa kwa wasaidizi wa kisheria wa kujitolea kwa muda wa siku 25," alisema Choaji.

Alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana. Lakini pia zilijitokeza changamoto baada ya kukamilika kwa awamu hiyo. Ikiwamo kutojua namna na jinsi wasaidizi wa kisheria wataweza kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria zinapatikana katika ubora unaostahili na namna upatikanaji wa msaada wa kisheria utakavyokuwa endelevu kwa masilahi mapana kwa jamii inayolengwa.

Choaji alilitaja lengo la mradi huo uliozinduliwa na kuwa ni wa awamu ya pili kuwa ni kuimarisha upatikanaji wa haki katika jamii kwa kuongeza ubora, uwezo na kuendeleza huduma za msaada wa kisheria, kuwezesha vitengo vya wasaidizi wa kisheria wilayani katika nyanja za uongozi na utawala, masuala ya fedha na namna ya kuandaa miradi, kuandika taarifa za utekelezaji na za fedha.
"Mradi huu unakusudiwa kutekelezwa kwa muda wa miaka minne kuanzia mwaka huu hadi 2020, katika mkoa huu wa Lindi, mradi utakelezwa katika wilaya zote sita na unakusudia kuzifikia kata zote 150 za mkoa huu," alibainisha Choaji.

Mtaalamu huyo wa LIWOPAC alisema ili dhamira hiyo ifanikiwe kikamilifu kupitia ufadhili wa LSF ambalo litafadhili shilingi 600.00 kwa kipindi chote cha miaka minne ya utekelezaji wa mradi hu, LIWOPAC ambayo inasimama kama asasi mama ya mkoa litakuwa linapokea shilingi 150.00, milioni kila mwaka na kuzigawa kila wilaya.

Ambapo kila kituo cha msaada wa kisheria cha wilaya(kitengo) kitapokea shilingi 8.00 milioni, kila mwaka.

Nae makamo mwenyekiti wa LIWOPAC, Abdallah Majumba, alisema viongozi wa serikali, hasa wa mitaa, dini na wadau wengine wanawajibu mkubwa wakutoa ushirikiano wakati wautekelezaji wa mradi huo ili kufikia malengo yanayokusudiwa.

Alisema kila mmoja anaowajibu wa kuchukia madhila na dhuluma za wazi na za siri zinazofanyiwa baadhi ya jamii hapa nchini, hasa wanawake na watoto ambao wamekuwa waathirika wakukosa haki za binadamu na haki za msingi.
"Tushikane na kushirikiane pamoja katika kuhakikisha utoaji na upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria katika jamii zetu unakuwa bora na endelevu," alisisitiza Majumba.

Kwa upande wake ofisa tawala wa wilaya hiyo, Stephano Mbije, alisema serikali inatambua na kuthamini kazi zinazofanywa na asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali na wahisani wa maendeleo katika kusaidia jamii kuhusu masuala mbalimbali. Ikiwamo haki za binadamu na haki za msingi.

Hivyo ipo tayari kutoa ushirikiano wa dhati katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo katika wilaya hiyo. 

Katika wilayani ya Nachingwea, kata zitakazo fikiwa na kunufaika katika awamu hii ya pili ya mradi huo ni Lionja, Nditi, Namanga, Stesheni, Ruponda, Namikango, Namapwiaya na Mnero Ngongo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top