Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akijaza fomu ya kujiunga na Mfumo wa Wote Scheme kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati alipotembelea Banda la PPF katika maonyesho ya Kilimo ya Nane Nane, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi. PPF imeuanzisha Mfumo huo wa hiari wa kujiwekea akiba kwa wale ambao wapo kwenye sekta rasmi na sekta binafsi kama Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Mama Lishe, Wajasiriamali na wote wanaojiajiri wenyewe wanapata fursa ya kuchangia na kupata faida kuu nne kama vile kupata bima ya afya, fursa ya mikopo ya maendeleo na mikopo ya Kujiendeleza kielimu pamoja na mafao ya uzeeni
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akijaza fomu ya kujiunga na Mfumo wa Wote Scheme kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati alipotembelea Banda la PPF katika maonyesho ya Kilimo ya Nane Nane, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Janet Ezekiel akishuhudia.
Tags
HABARI ZA KITAIFA