Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan Akiwahutubia wananchi waliohudhuria katika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi wakati wa Ufungaji wa maonyesho ya Nane nane.
Waziri wa kilimo uvuvi na maliasili wa serikali ya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed akiwahutubia wananchi wa Lindi na Mtwara waliojitokeza kushuhudia ufungaji wa maonyesho ya wakulima Nane nane yaliyofanyika viwanja vya Ngongo - Lindi.
Viongozi Mbalimbali wa Serikali wakifuatili kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassani wakati wa ufungaji wa Maonyesho ya kilimo ya Nane nane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Serikali imeahidi kuendelea kubana matumizi na kupambana na ufisadi ili nchi iweze kufikia uchumi wa kati kama ilivyokusudiwa.
Hayo yameelezwa leo na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi wakati wa Ufungaji wa maonyesho ya Nane naneambayo yamefanyika katika viwanja hivyo.
Alisema ilikufikia uchumi wa kati serikali imejizatiti kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi rushwa na ukwepaji kodi. Sambamba na kukusanya kodi, iliiweze kutoa huduma bora na zinazostahiki kwa wananchi wake, ilikufanikiwa kufikia uchumi wa kati kama ilivyoahidiwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Hivyo serikali inapambana na ufisadi kuondoa matumizi yasiyo ya lazima ili kubana matumizi na kutovumilia uvivu na uzembe, Hivyo wananchi wakiwamo wakulima wafugaji nao wanawajibu wa kuisadia serikali kwa kujiepusha na kukemea vitendo vya Rushwa, Huku akitoa wito kwa wananchi kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao kwa sababu malighafi zinazotarajiwa kutumika viwandani zinatokana na kilimo, ufugaji, uvuvi na maliasili nyingine.
kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuimarisha na kuwa viwanda vingi vidogovidogo ili kuongeza thamani ya mazao kwa ajili kutengeneza soko mazuri ya ndani na nje ya bidhaa zitakazo zalishwa.
Makamo huyo wa Rais ambaye amehudhuria maonyesho hayo kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe na kuwa makamo wa rais alisema serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji endelevu wa chakula na mapinduzi ya kilimo, kutoka kilimo cha kujikimu nakuwa kilimo cha biashara.
Alisema serikali imetengeneza mikakati ili sekta ya kilimo iweze kuwa na tija ikiwemo kuanzishwa kwa benki ya kilimo ambayo miongoni mwa majukumu yake ni kuvijengea uwezo vikundi vya kilimo kuongeza bajeti ya kilimo, kurahisisha mipango ya utendaji na kuongeza idadi ya maofisa ugani.
Aidha katika kuhakikisha migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji inatoweka, amevitaka vijiji kuingia kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi ili vitenge maeneo kwa matumizi mbalimbali ya kibinadamu ikiwamo maeneo ya kilimo na ufugaji.
Ambapo pia aliahidi kutafuta uwezekano wa kuziondoa kodi katika sekta hizo, Hatua ambayo inafuatia baada ya serikali kuondoa ushuru katika pembejeo za kilimo, vifaa vya uvuvi na dawa za mifugo.
Nae waziri wa mifugo, Charles Tizeba alisema japokuwa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi zimekuwa zikiongeza vipato na kuondoa umaskini, lakini imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi, hivyo kupunguza uzalishaji wa mazao.
Alisema ilikubaliana na hali hiyo, wizara yake kwa kutumia wataalamu wa kilimo inafanya tafiti za kubainimbegu bora na zitakazo toa mazao mengi, kwa upande wake waziri wa kilimo uvuvi na maliasili wa serikali ya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed alitoa wito kwa wakulima na wataalamu hasa waliopo kwenye taasisi wazalishe kwa ajili ya kulenga mazao ya Biashara na kutafuta masoko.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.