NIJUZE NIJUZE Author
Title: MH. HAMIDU BOBALI AITAKA SERIKALI KUTOTUMIA NGUVU KWA WAVUVI, LA SIVYO WATENGENEZE LESENI ZA MBAO (+Audio)
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mbunge wa Mchinga Mh. Hamidu Bobali ameitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kuacha mpango wake wa kutumia jeshi katika kufanya...
Mh. Hamidu Bobali
Mbunge wa Mchinga Mh. Hamidu Bobali ameitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kuacha mpango wake wa kutumia jeshi katika kufanya doria kwa wavuvi nchini kwani Wavuvi wanadhalilishwa na kupigwa kwa kile kinachosemwa kuwa hawana leseni. 

Hivyo ameitaka serikali kutengeneza leseni za Mbao ili wavuvi hao weweze kutembea nazo hata wakiwa baharini pindi wakiwa wanavua ili zisiweze kuharibika kwani Leseni za sasa ni za karatasi.

Pia Bobali amezungumzia suala la zao la Ufuta katika Mkoa wa Lindi, amesema kuwa Mkoa wa Lindi ndio mkoa wa kwanza kuzalisha zao hilo kwa wingi hapa nchini lakini hadi sasa hakuna Bei elekezi ya zao hilo. 

Kufuatia jambo hilo Choma choma wameweza kutumia mwanya huo kuwa kandamiza wakulima wa zao hilo kwa kununua zao hilo kwa bei ya kuanzia Tsh 1300/= na 1800/= 
Amesema kuwa kwa hali hii inaumiza wakulima wa zao hilo hivyo ameitaka serikali kutangaza Bei elekezi ili kuwanusuru wakulima wa zao hilo.

UNAWEZA KUMSIKILIZA HAPA AKIZUNGUMZA.

About Author

Advertisement

 
Top