HATIMAE HOSPITALI YA RUFAA YA SOKOINE YAREJESHA HUDUMA YA X-RAY

Hospitali ya Rufaa Sokoine
Kutokana na malalamiko mengi ya baadhi ya wakazi wa Lindi kuhusiana na Hospitali ya Rufaa Sokoine iliyopo Mkoani hapa kutokuwa na huduma muhimu ya X-Ray hatimaye katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Bw, RAMADHANI KASWA, amesema tatizo hilo kwa sasa halipo na kwamba kifaa hicho kinafanya kazi kama kawaida.

Akiongea na Lindiyetu.com Bw, Kaswa amesema kulikuwa na changamoto hiyo kwa kipindi cha nyuma, lakini kwa sasa kifaa hicho kimerekebishwa na sasa huduma hiyo inaendelea kutolewa na inapatikana kwa ufasaha. Pia amesema kuwa Hospitali hiyo inajiandaa kununua Portable X-Ray mnamo mwezi wa Nane mwaka huu, ambayo itakuwa ikitumika kwa dharula.


MSIKILIZE HAPA AKIONGELEA TATIZO HILO.
Previous Post Next Post