
Miongoni mwa waliovuliwa uongozi ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Saad Kusilawe alisema uamuzi huo umetokana na kikao cha Halmashauri Kuu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Saad Kusilawe alisema uamuzi huo umetokana na kikao cha Halmashauri Kuu.
Wengine waliovuliwa madaraka na vyeo vyao katika mabano ni Edward Lubinza (Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya) na Ng’honge Nkwabi (Kamanda wa UVCCM ) ambao wote ni wa Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Pia aliwataja wengine na vyeo vyao kwenye mabano ni Charles Nkwabi (Katibu Kata ya Kisuke) kata ya Ngogwa, Wilfred Sazia (Mwenyekiti Kata Ngogwa), Samwel Gachu ambaye ni Katibu Mwenezi kata ya Isaka.
Viongozi wengine waliovuliwa nyadhifa ni Peter Kigingi (Mwenyekiti Kata ya Bukomela) na Japhet Mabula ambaye ni Katibu Kata ya Mjini Kahama.
Kusilawe alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM Toleo la mwaka 2012 Ibara ya 93, Kifungu kidogo cha 14 kinatoa mamlaka kwa Halmashauri Kuu ya Mkoa, kumchukulia hatua mwanachama yeyote atakayedhihirika kukosa sifa ya chama hicho.
Tags
HABARI ZA KITAIFA