HABARI ZA HIVI PUNDE:: FIFA YAMTIMUA KAZI NAIBU KATIBU MKUU WAKE

Shirikisho la soka duniani FIFA limemtimua kazi naibu katibu mkuu wake Markus Kattner kwa kujihusisha na matumizi mabaya na ya siri ya mamilioni ya dola.
Markus Kattner
Kattnet raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 45 alikuwa akishikilia kwa muda nafasi ya katibu baada ya aliyekuwa katibu Jerome Valcke kutimuliwa kazi kutokana na kashfa za rushwa.

Kaimu huyo wa nafasi ya katibu alifutwa kazi mara moja baada ya bodi ya uchuguzi ya ndani ya Fifa kugundua kuwa alikuwa akikiuka na kuvunja kanuni katika majukumu yake.

Bodi imetoa ushahidi wa kutosha na vielelezo vinavyoonyesha mapungufu katika majukumu yake ikiwemo kutumia pesa za ziada katika kuamua kiasi gani rais, katibu mkuu na naibu katibu mkuu walipwe.
Previous Post Next Post