Klabu ya Yanga imeshindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Al Ahly ya Misri kwenye mchezo wa klabu bingwa Afrika uliopigwa kwenye uwanja wa taifa.

Al Ahly walikuwa wakwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 9 kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Amri Gamal ambaye aliukwamisha wavuni mpira wa adhabu ndogo ambao haukuokolewa na mabeki wa Yanga.
Dakika ya 19 Yanga walipata bao la kusawazisha baada ya beki wa Al Ahly kujifunga wakati akijaribu kuokoa krosi iliyopigwa na winga wa kimataifa wa Niger Issoufou Boubacar na kuipa Yanga goli la kusawazisha.
Timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa sare ya kufungana bao 1-1 matokeo ambayo yalidumu kwa dakika zote za mchezo.
Yanga watasafiri kwenda Misri kwa ajili ya kucheza mchezo wa marudiano ambao utachezwa kati ya April 19 au 20. Mchezo huo ndiyo utaamua timu ipi itakayosonga mbele ya mashindano.

Kivutio kikubwa kwenye mechi hiyo ilikuwa ni mashabiki wa Al Ahly ambao walikuwa wakiimba na kupiga ngoma kuishangilia timu yao kwa dakika zote za mchezo kitu ambacho mashabiki wa kibongo wanatakiwa kujifunza.
Tags
SPORTS NEWS