

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya mashuka hayo, Mwenyekiti wa SACCOS hiyo, Bi Somoe Ismail Nguhwe, ameeleza kuwa msaada huo umelenga kuisaidia hospitali hiyo ya rufaa kukidhi mahitaji ya mashuka ili Kupunguza Tatizo lililopo.

Aidha, Bi Nguhwe alisema kuwa Chama hicho cha wafanyakazi wa Tanesco wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa hospitali na vituo vingi vya afya nchini vinakabiliwa na uhaba wa mashuka pamoja na vifaa tiba mbalimbali.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Saccos Hiyo mkoa wa Lindi, Mohamed Chembe akimkaribisha Mwenyekiti wake wa Taifa Kukabidhi Msaada Huo alibainisha Kuwa fedha zinazotumika kununulia mashuka ya misaada, zinatokana na faida ambayo SACCOS inapata baada ya mahesabu ya mwaka kukaguliwa na kutoa gharama na matumizi yote.
Akitoa shukurani baada ya Kukabidhiwa Msaada huo, Muuguzi Kiongozi wa Wodi ya Akina mama na Magonjwa Mchanganyiko Bi Magdalena Mmuni aliishukuru saccos ya Tanesco na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa mashirika mbalimbali na wadau wa sekta ya afya kuiga hatua iliyochukuliwa na saccos ya Tanesco ili kuzipunguzia hospitali makali ya gharama za uendeshaji.
Sambamba na Utoaji wa Msaada Huo wa Mashuka 150 Baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco pia walipata Fursa ya Kuona wagonjwa Mbalimbali waliolazwa katika Hospital Hiyo.




Tags
HABARI ZA KITAIFA