ANDY CARROLL AZIMA NDOTO ZA UBINGWA WA ARSENAL MARA BAADA YA KUTOKA SARE YA 3 - 3

HETITRIKI ya ndani ya Dakika 9 ya Straika wa West Ham Andy Carroll Leo huko Upton Park imekuwa pigo kubwa kwa Arsernal katika mbio zao za Ubingwa walipotangulia 2-0 na kuambua Sare ya 3-3 na West Ham.
Andy Carroll

Arsenal walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 18 baada ya pasi ya Iwobi kumkuta Mesut Ozil aliemalizia vizuri na la pili kufungwa Dakika ya 35 kupitia Alexis Sanchez kwa pasi iliyotoka kwa Iwobi.

West Ham walifufuka na kufunga Bao lao la kwanza Dakika ya 44 kwa Kichwa cha Andy Carroll alieunganisha krosi ya Cresswell na kupata Bao la Pili Dakika ya 47 kupitia tena Andy Carroll ambae aliunganisha Mpira wa Kona iliyoooshwa na kumkuta Mark Noble alieurudisha tena Golini na kumkuta Carroll aliepiga Shuti la kwanza ambalo lilizuiwa na kuachia kigongo cha pili na kumparaza Beki na kumhadaa Kipa Ospina.

Hadi Mapumziko, West Ham 2 Arsenal 2.

Dakika ya 52 Carroll alipiga Bao la 3 na kukamilisha Hetitriki yake ya ndani ya Dakika 9 tu.
Arsenal walisawazisha na kuambua Sare ya 3-3 katika Dakika ya 70 kwa Bao la Laurent Koscielny.

Matokeo haya yamezibakisha Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Leicester City na West Ham kuwa Nafasi ya 6.

VIKOSI: West Ham: Adrian; Tomkins, Reid, Ogbonna, Cresswell; Kouyate, Noble; Antonio, Lanzini, Payet; Carroll.
Akiba: Randolph (GK), Hendrie, Oxford, Obiang, Moses, Valencia, Emenike.

Arsenal: Ospina; Bellerin, Gabriel, Koscielny, Monreal; Coquelin, Elneny; Sanchez, Ozil, Iwobi; Welbeck.
Akiba: Cech, Gibbs, Mertesacker, Chambers, Ramsey, Giroud, Walcott.

REFA:Craig Pawso 

RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND
Jumapili Aprili 10
1530 Sunderland v Leicester
1800 Liverpool v Stoke
1800 Tottenham v Man United
Jumatano Aprili 13
2200 Crystal Palace v Everton

MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND

POSLPCLUBPWDLGFGAGDPTS
1(1)Leicester City32209355312469
2(2)Tottenham Hotspur321711457253262
3(3)Arsenal32178755332259
4(4)Manchester City31166956322454
5(5)Manchester United31158839271253
6(6)West Ham United321313652401252
7(7)Southampton32138114133847
8(8)Stoke City32138113639-347
9(9)Liverpool3012994641545
10(10)Chelsea31111194941844
11(11)West Bromwich Albion311010113037-740
12(12)Everton30911105142938
13(13)Bournemouth32108143854-1638
14(14)Watford31107143036-637
15(15)Swansea City32910133342-937
16(16)Crystal Palace3197153442-834
17(17)Norwich City3287173556-2131
18(18)Sunderland3169163655-1927
19(19)Newcastle United3167183158-2725
20(20)Aston Villa3237222262-4016
POSLPCLUBPWDLGFGAGDPTS
Previous Post Next Post