RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AMJULIA HALI WAZIRI WA ZAMANI MZEE SUMAYE HOSPITALI YA MUHIMBILI (+VIDEO)

Frederick Sumaye
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye na Mama Esther Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Jumatatu Januari 11, 2016.
Waziri huyo wa zamani wa Tanzania ameweza kumshukuru Rais Magufuli kwa kwenda kumjulia Hali..
"Nimeshukuru sana Rais kuja kunitembelea hapa ni jambo kubwa, nimeshtuka kwa sababu sikutegemeana sikupata taarifa yoyote…. namshukuru Rais Magufuli kwa upendo wake, anaonesha kujali sana watu wake." 
Frederick Sumaye

 Amesema Frederick Sumaye na kuongeza;
"Naendelea vizuri, hali yangu ni nzuri natumaini baada ya muda mfupi nitatoka hospitali"

Previous Post Next Post