UPDATES: MAALIM SEIF ASEMA KUWA HATAKUBALI UCHAGUZI KURUDIWA, UCHAGUZI KUFUTWA NI BATILI.

Maalim Seif Sharif Hamad
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad leo amezungumza na wahariri wa vyombo vya habari juu ya Mustakabali wa hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na hatua ambayo imefikiwa hadi hivi sasa.

Maalim anasema tume haina mamlaka ya kutengua matokeo bali ina mamlaka ya kurudia kuhesabu kura. Mwenyekiti wa tume Zanzibar alienda kinyume cha katiba kwa kufanya maamuzi bila kushirikiana na tume. 
Maalim anasema Katiba inasema "kila uamuzi wa tume ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi". 
Anasema katiba imetumia neno 'Lazima' na mwenyekiti kwenda kinyume inafaa kuchukuliwa hatua.

ENDELEA KUWANASI KWA TAARIFA ZAIDI
Previous Post Next Post