NIJUZE NIJUZE Author
Title: CHADEMA WAMKATAA MEYA NA NAIBU WAKE, WAFANYA VURUGU NA KUTAKA WAJIUZURU
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
KIKAO cha Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa kimevunjika baada ya wajumbe wa Chadema kuwataka Meya Justine Mal...
Chadema
KIKAO cha Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa kimevunjika baada ya wajumbe wa Chadema kuwataka Meya Justine Malisawa (CCM) na Naibu wake, Anthony Choma (CCM) wajiuzulu wakidai kuwa hawakuchaguliwa kihalali.

Malisawa alipata wakati mgumu kuongoza kikao hicho hata kushindwa kukifungua kila alipojaribu kufanya hivyo, kwani madiwani wa Chadema walisimama na kupiga meza kwa nguvu huku wakiimba kwa sauti ya juu na kusababisha maelekezo aliyokuwa akiyatoa meya huyo yasisikike.

Huku wakiimba kwa kulitaja jina la Simbachawene, walisema hawana imani na Meya na Naibu wake, hivyo kumlazimisha Meya kuacha kuzungumza na kukaa kitini. Walikuwa wakitaja jina la Simbachawene katika wimbo wao wakimaanisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.

Ndipo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Hamidu Njovu ambaye kwa wadhifa wake huo ni Katibu wa kikao hicho aliposimama na kuwaongoza wajumbe akiwasisitiza wafuate kanuni, sheria na taratibu zinazoongoza vikao vya mabaraza ya Manispaa.

Hata hivyo, madiwani hao walikaidi wakisisitiza hawamtambui Meya huyo na Naibu wale wakidai wajiuzulu ili ateuliwe mwenyekiti wa muda atakayekuwa akiongoza vikao vya baraza hilo hadi hapo mgogoro huo utapopatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Hoja za madiwani hao wa Chadema, walisisitiza hawawatambui viongozi hao wawili kwa kuwa uchaguzi uliofanyika Desemba 16, mwaka jana uliowaingiza madarakani ulikuwa batili kwa sababu CCM waliingiza watu ambao hawakuwa na sifa ya kupiga kura.

Waliwataja wajumbe hao kuwa ni wabunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (Katavi), Mwanne Nchemba (Tabora) na Bupe Mwakang’ata kutoka Jimbo la Kwela wilaya ya Sumbawanga Vijijini.

About Author

Advertisement

 
Top