SEREKALI YATOA ONYO KWA VYOMBO VYA HABARI VITAKAVYOTUMIA RAMANI YA TANZANIA ISIYO RASMI

Ramani rasmi ya Tanzania
Ramani rasmi ya Tanzania iliyotolewa na Serikali mwaka 2013

SERIKALI imesema itavichukulia hatua vyombo vya habari pamoja na watu watakaobainika kutumia ramani ya Tanzania ambayo sio sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, alisema kumekuwa na matumizi ya ramani ya Tanzania ambayo inaonesha Ziwa Nyasa lipo katika nchi ya Malawi pekee huku Tanzania ikionekana kutohusika kabisa katika ziwa hilo.

Mwambene alisema ramani sahihi ya Tanzania inaonesha Ziwa Nyasa lina mpaka katikati ambao unaonesha umiliki wa ziwa hilo upo upande waTanzania na Malawi. Aliongeza kuwa hivi karibuni kumekuwa na vyombo vya habari ambayo vimekuwa vikitumia ramani hiyo ambayo sio ramani sahihi.

“Ni vibaya sana vyombo vya habari kutumia ramani ambayo sio sahihi kwani kufanya hivi ni kuharibu utaifa na utambulisho wetu,” alisema Mwambene.
Previous Post Next Post