WANACHAMA WA CUF WATIFUANA HUKO TANGA, KISA HIKI HAPA

Wanachama CUF
Wanachama zaidi ya mia moja wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Pangani Mkoani Tanga wametishia kujeresha kadi zao za chama na kujiunga na vyama vingine vya siasa..

Madai ya wanachama hao ni kutaka kurejeshwa kwa jina la aliyekuwa mbunge wa viti maalumu Amina Mwidau kwa kuwa ndiye aliyeshinda kwenye kura za maoni na kuliondoa jina na Saumu Sakala aliyeshika nafasi ya pili kwenye mchakato wa kura za maoni.

Wanachama hao wanasema chama hicho kinaweza kufa kama uongozi wa juu hautasikia kilio hicho chenye maslahi ya kisiasa katika wilaya ya Pangani.

Katubu wa chama hicho wilaya ya Pangani Ramadhan Hadadi amesema waliofanya kazi hiyo ni Baraza la uongozi la chama hicho Taifa.

Amina Mwidau licha ya kugombea viti maalumu kupitia chama hicho ,aligombea kwenye jimbo la Pangani na kuangushwa na mgombea CCM Jumaa Aweso.
Previous Post Next Post