Jeshi la polisi mkoani Tanga linamshikilia aliyekuwa askari wake Bw Ansoni Temu F 785 miaka 46 kwa tuhuma za kushawishi na kuchukua rushwa kutoka kwa dereva wa gari katika kijiji cha Kilumbo wilayani Handeni mkoani Tanga
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Tanga Zuberi Mwombeji askari huyo anachukuliwa hatua za kisheria na tayari ameshafukuzwa kazi na kwa sasa yupo mahabusu akisubiri kupelekwa mahakamani
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa saba mchana kwenye eneo la barabara ya Segera - Chalinze, na leo asubuhi jeshi hilo limetangaza kuwa limemfukuza kazi na hatua za kisheria za kumfikisha mahakamani zinafanyika