NIJUZE NIJUZE Author
Title: OMMY DIMPOZ AWAPONDA MA MODELS WA TANZANIA, ASEMA SIO PROFFESIONAL....!!!
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Msanii Ommy Dimpoz amesema sababu ya wasanii kufanya kazi na models wa nje wanapoenda kufanya video ni kutokana na models wa nje kuwa prof...
Msanii Ommy Dimpoz amesema sababu ya wasanii kufanya kazi na models wa nje wanapoenda kufanya video ni kutokana na models wa nje kuwa proffesional zaidi kuliko wa hapa nyumbani.
Ommy Dimpoz
Ommy Dimpoz
Ommy Dimpoz ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Radio Moja ya hapa nchini, na kusema kuwa kuna baadhi ya vitu models wa hapa nyumbani wanashindwa kufanya kutokana na maadili kutoruhusu.

"Mara nyingi models wa nje wako proffesional wanaweza kucheza character zote ambazo wamepangiwa, huku unajua kidogo kuna scene ambazo mtu anatakiwa acheze lets say amevaa swimming costume, unajua huku kumpata msichana ambaye anaamua kujiachia hivyo ni wachache sana, hata kama ikitokea mnaweza mkajikuta msichana huyo huyo atatumika kwenye video za watu wote", alisema Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz amesema mbali na hayo pia wanafanya hivyo kwa kupunguza gharama za kusafiri na watu wengi, kwani huko wanapatikana kwa urahisi zaidi.
"Kikubwa ni kupunguza gharama, huko wako kibao utawakuta wengi sana, kwa hiyo ndo mana nasema hiyo nayo inachangia, pia ni vigumu kuondoka na watu wote kwenda nao kushoot nao nje, kwa sababu kule unawapata kwa bei rahisi alafu ukilipia video ina maana unalipia kila kitu", alisema Ommy Dimpoz.

About Author

Advertisement

 
Top