Wananchi wa halmashauri ya Mtwara vijijini wamepaza sauti zao kuulalamikia uongozi wa Wakala wa Usajili wa Vizazi na Vifo (RITA) mkoa wa Mtwara, kutokana na usumbufu wanaoupata katika ufuatiliaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wachanga.
Wamesema, ofisi hiyo imeanza kufungwa tangu mwezi Agosti mwaka huu baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais uliofanyika mwezi Oktoba, kutokana na muhusika kuamua kujiingiza katika siasa.
Kwa upande wake, afisa tawala wa wilaya ya Mtwara, ambako ndiko kuna ofisi hiyo, Edith Shayo, amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao na kusema kuwa mara kadhaa anajitahidi kutoka na kuwaeleza changamoto walizo nazo zinazosababisha ofisi kufungwa na wao kukosa huduma.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi. Emmy Hudson akitoa maelezo kuhusu ushiriki wa RITA katika tathmini
Wakizungumza na mwandishi wakiwa nje ya ofisi hiyo, wamesema mara kadhaa wamekuwa wakitekeleza bila mafanikio, maagizo wanayopewa na wahusika kwa kuwapangia tarehe za kupatiwa vyeti hivyo lakini inashindikana kutokana na ofisi kuwa inafungwa kila wanapofika na kukosa mtu wa kuwahudumia.Wamesema, ofisi hiyo imeanza kufungwa tangu mwezi Agosti mwaka huu baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais uliofanyika mwezi Oktoba, kutokana na muhusika kuamua kujiingiza katika siasa.