BODI YA KOROSHO KUTOTOA VIBALI KWA WANUNUZI WASIO WAAMINIFU

Bodi ya Korosho Nchini imesema haitatoa vibali vya kusafirisha korosho kwa wanunuzi wa zao hilo wanaopenda kuvuruga Mfumo.
Mfaume Juma
Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Mfaume Juma

Bodi ya Korosho Nchini imesema haitatoa vibali vya kusafirisha korosho kwa wanunuzi wa zao hilo wanaopenda kuvuruga Mfumo wa Stakabadhi wa Mazao Ghalani na kununua kwa njia isiyo halali.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara, Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Mfaume Juma, amesema bodi hiyo pia itachukua hatua za kisheria kwa wanunuzi au makampuni yatakayokiuka utaratibu huo na kuwanyonya wakulima.

Mpaka sasa wiki tano zimepita tangu minada ya korosho ianze kufanyika msimu huu, ambapo korosho zilizokusanywa katika maghala makuu na kuuzwa kati ya tarehe mbili Oktoba na tarehe nane mwezi huu ni tani 57,252,450, korosho hizo zimeuzwa kwa bei za ushindani kati ya shilingi 2,407/= hadi shilingi 2,640/= kwa kilo moja.
Previous Post Next Post