Unknown Unknown Author
Title: MSANII RAY KIGOSI AWASTUA KISHAPU, AWAAMBIA UPINZANI BADO SANA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Muigiza filamu maarufu, Kajala Masanja, akiongea katika mkutano wa kampeni za Nimes'tuka, uliofanyika katika jimbo la Kishapu mchan...
Nimes'tuka Kishapu
Muigiza filamu maarufu, Kajala Masanja, akiongea katika mkutano wa kampeni za Nimes'tuka, uliofanyika katika jimbo la Kishapu mchana wa leo, kulia ni Ray Kigosi

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
Msanii Nguli wa filamu nchini, Ray Kigosi, amewaambia watanzania leo kuwa makini na kusikiliza sera na kuachana na mihemko ya kisiasa itakayopelekea wao kufanya maamuzi watakayoyajutia baadae.

Kigosi ameyasema hayo alipokuwa katika moja ya mikutano inayoendeshwa na kundi la wasanii lenye kauli mbiu ya Nimestuka, katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kundi hilo inayopita kijiji kwa kijiji katika kuhakikisha kwamba wanawaelimisha vijana wenzao kuhusiana na usikilizwaji wa sera na mapokeo ya demokrasia kwa jamii.

Awali akiongea kabla ya kuwakaribisha wenzake 12 alioandamana nao, Kigosi amesema yeye alipokuwa Ukawa alikuwa akishuhudia vijana wakihamasishwa kupinga hata mambo yanayoonekana kuwa na tija yaliyofanywa na serikali jambo ambalo yeye mwenyewe aliliona kuwa ni upotoshwaji wa wazi wazi.
"Naamini kuwa mpinzani, sio kupinga kila kitu, walipaswa pia kutufundisha jinsi ya kukabiliana na maisha kama vijana, lakini nikaja kugundua nimekosea sana kuacha kuungana mkono na Magufuli", alikiri Kigosi.

Nimes'tuka Kishapu
Mchekeshaji Kitale, akiongea katika Mkutano wa Kampeni ya Nimes'tuka, inayoendeshwa na wasasnii wa filamu na muziki wa kizazi kipya, uliofanyika katika jimbo la Kishapu jioni hii
Nimes'tuka Kishapu
Inspekta Haroun, mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya akitoa burudani kwa wakazi wa jimbo la Kishapu baada ya mkutano wao wa kampeni ya Nimes'tuka, inayoendeshwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, wanaokiunga mkono Chama cha Mapinduzi
Nimes'tuka Kishapu
Mchekeshaji Mboto, naye ni mmoja kati ya wasanii wanaoendesha kampeni za Nimes'tuka, hapa akiongea na wananchi wa jimbo la Kishapu, mkoani Shinyanga
Nimes'tuka Kishapu
Muigizaji Skyner Ally naye akimwaga sera zake katika kampeni za Nimes'tuka
Nimes'tuka Kishapu
Miss Tanzania 2014, Lilian Kamanzima, akiongea na wananchi wa jimbo la Kishapu jioni ya leo katika mkutano wa kampeni za Nimes'tuka
Nimes'tuka Kishapu
Mikono juu... 
Nimes'tuka Kishapu
Ray Kigosi akimwaga sera...
Nimes'tuka Kishapu
Msanii wa vichhekesho, StanBakora naye akiongea yake Kishapu leo
Nimes'tuka Kishapu

About Author

Advertisement

 
Top